,
Msemaji wa kampuni ya M-Bet Tanzania David Malley (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi watano wa droo ya Perfect 12 walioshinda kwa kubashiri kwa usahihi matokeo ya michezo 12 kati ya 17 za ligi mbalimbali duniani.
…,.,……………………………
Dar es Salaam. Jumla ya wa wanamichezo watano wameshinda kiasi cha Sh86,844, 530 baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 za ligi mbalimbali duniani kupitia droo ya Perfect 12 ya kampuni ya M-Bet.
Washindi hao wamepatisakana katika droo ya M-Bet iliyofanyika Januari 6 jijini kwa mujibu wa msemaji wa kampuni ya M-Bet Tanzania David Malley.
Malley aliwataja washindi hao kuwa ni Charles Hamis, Isihaka Mombo (Njombe), Titus Mguli (Njombe), Eric Mosha (Tanga) na Baltazary Saunary wa Arusha.
Malley alisema kuwa kupatikana kwa washindi hao kunafanya droo ya 101 tokea kuanzishwa kwa Pefect 12 ambayo ni nyumbaya mabingwa.
Alisema kuwa M-Bet inajivunia kuendelea kubadili maisha ya Watanzania kupitia michezo yake mbalimbali na kuwaomba watanzania wenye vigezo vya kufanya hivyo kuanza kujaribu bahati yao.
“Sisi tunaendelea kuwa nyuma ya mabingwa na kuwainua vipato watanzania, mpaka sasa kuna washindi wengi wamefaidika na michezo yetu na kuweza kubadili maisha yao,” alisema Malley.
Mmoja wa washindi hao, Charles Hamis kutoka Lindi alisema kuwa amefurahi sani kushinda kiasi cha fedha hicho kwa kutumia Sh1,000 tu kubahatisha.
Hamisi ambaye shabiki wa timu ya Simba na Manchester United alisema kuwa awali alidhani kuwa michezo ya kubahatisha ni ‘dili’ lakini baada ya kuona mashabiki kibao wakishinda kupitia M-Bet, naye aliamua kubashiri.
“Sikukata tamaa kutokana na ukweli kuwana watu wangu wa karibu walikuwa wanashinda kiasi cha fedha kupitia mchezo wa Perfect 12, niliamini kuwa kuna siku nami nitashinda,” alisema Hamis.
Kwa upande wake, Mguli ambaye ni shabiki wa Simba na Chelsea alisema kuwa atatumia fedha hizo kuendeleza biashara zake na kuinua kipato.