Waziri wa Viwanda na Biashara Geoffrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Wakala wa Vipimo jana jijini Dar es salaam kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe.
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA ,Stella Kahwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo WMA wakiwa katika kikao hicho.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Geoffrey Mwambe amesema changamoto kubwa iliyopo katika bidhaa nyingi za viwanda vya ndani ni pamoja na kutokuwa na vipimo sahihi katika baadhi ya bidhaa wakati zinapofungashwa.
Pia amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wakala wa Vipimo nchini(WMA),watahakikisha kuwa na mkakati wa kwenda katika maeneo ya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kuwasimamia na kuangalia bidhaa zinazozalishwa kama zinaviwango vinavyostahili.
Akizungumza hayo juzi wakati walipotembelea ofisi ya wakala wa vipimo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukuonea utendaji kazi wa watumishi wa Ofisi hiyo na kujifunza wanachokifanya kwa kuwapa mawazo yao.
Alisema kuna baadhi ya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali sio waaminifu,akitolea mfano Mfuko wa Saraju unatakiwa kuwa na kilo 50 wazalishaji wanaweka kilo 48 hadi 46,katika nondo inatakiwa kuwa na
urefu wa futi 40 ila wazalishaji wanaweka futi 38.5 ambapo wanunuzi wanaonunua hawajui kama bidhaa hizo vipimo vyake umepungua.
Mwambe alisema wamejipa kuhakikisha kumfatilia katika maeneo ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali na kuchukua sample za bidhaa hizo na kuzipima endapo watakuta zinadosali za ujazo usio sawa watahakikisha wanakomesha tabia hiyo na kama tatizo lipo kwenye mitambo yao upimaji watahakikisha wanazirekebisha mashine zao.
“Tunataka kuhakikisha wanazihakiki bidhaa zao sio nasubiri hadi ziende sokoni na kuanza kupigana faini kutokana na kutuweka ujazo sahihi,huku wananchi wanakuwa tayari wameumia,”alisema na kuongeza
“Pia WMA inatakiwa kuwa wabunifu na kuja na mbinu mpya kila wakati kuhakikisha inasaidia wafanyabiashara na kama kunatatizo waanze kutengeneza katika vyanzo vya ndani na sio katika soko linaloweza kuleta tatizo,”alisema Waziri Mwambe
Alisema Wizara yake ni walezi wa biashara za viwandani wanataka kukuza bidhaa nyingi hivyo wakikumbushana faida ya viwanda vingi na bidhaa nyingi nchini ikiwemo kuongeza soko la ajira.
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA ,Stella Kawha
alisema vipimo ni viwanda hivyo wanapokea maelekezo yote watahakikisha wanayafanyia kazi kwa haraka na weledi zaidi.