Mkurugenzi wa Kanda wa TDL,Davis Deogratias (Kulia),Mkurugenzi wa Mauzo Kanda ya Kusini Mwesige Mchuruza na Meneja wa Fedha Fredy Kayanda wakigongea glasi za mvinyo wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TDL wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Mameneja Waandamizi wa TDL wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kanda, Davis Deogatias (wa pili kushoto) wakionyesha chapa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Wafanyakazi wakiendelea kuburudika
*********************************************************
Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama Konyagi iliyopo chini ya kampuni ya TBL Group mwishoni mwa wiki alisherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwakwe,hafla hiyo iliyojumuisha wafanyakazi na wadau mbalimbali ilifanyika makao makuu yake makuu Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kanda wa TDL, Davis Deogratias, alisema katika miaka 50 ya kampuni hiyo imepata mafanikio makubwa na aliwapongeza wafanyakazi ,Serikali na wadau ambao kwa nyakati tofauti wamefanikisha kupatikana mafanikio haya ambayo yapo hadi sasa.