******************************************
Baada ya kutoka sare katika mechi ya kwanza Yanga imefanikiwa kutoka na pointi tatu muhimu dhidi ya Namungo katika michuano ya Mapinduzi Cup yanayoendelea Visiwani Zanzibar baada ya kuichapa Namungo bao 1-0.
Bao la pekee la Yanga liliwekwa kimyani na Kiungo wao Zawadi Mauya mnamo dakika ya 24 ya mchezo.
Yanga ilifanya mabidiliko kadhaa ya wachezaji na kuwapumzisha wachezaji ambao walianza katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo.