Home Michezo SIMBA YAANZA VEMA MAPINDUZI CUP, YAICHAKAZA CHIPUKIZI MABAO 3-1

SIMBA YAANZA VEMA MAPINDUZI CUP, YAICHAKAZA CHIPUKIZI MABAO 3-1

0

************************************************

Klabu ya Simba leo imeshuka dimbani kukipiga dhidi ya Chiukizi Fc ya Visiwani Zanzibar katika michuano ya Mapinduzi Cup na kubuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo huo.

Mabao manne yaliyofungwa leo Uwanja wa Amaan yalifunguliwa na nyota wa Chipukizi Fakhi Mwalimu dakika 36 huku Simba ikiweka usawa kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya 45.

Miraji Athuman ambaye amekuwa nyota wa mchezo wa leo kwa kusepa na laki mbili alipachika mabao mawili leo kipindi cha pili.

Alianza kupachika bao la pili kwa kichwa dakika ya 53 kwa pasi ya Kagere na lile la pili alipachika dakika ya 83 na kuifanya Simba kuanza kwa ushindi leo.