Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Gerald Mweli akizungumza na maofisa elimu, walimu wakuu na wakuu wa sekondari wa halamshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza lipofanya ziara ya siku moja katika halmashauri hiyo. Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Gerald Mweli akikagua vyumba vya madarasa katika sekondari ya Nyehunge halamshauri ya Buchosa wilayani Sengerema jijini Mwanza alipofanya ziara ya siku moja katika halmashauri hiyo.Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Gerald Mweli akizungumza na wnanchi na baadhi ya watumsihi bada ya kukagua ujenzi wa vyumba vinane na matundu 10 ya vyoo katika sekondari mpya ya Sukuma inayojengwa kwa nguvu za wananchi ka kushirikiana an halamshauri hiyo wilayani Sengerema mkoani Mwana jana.
*****************************************************
OR-TAMISEMI, Mwanza
Naibu Katibu Mkuu Elimu, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Gerald Mweli amewataka maofisa elimu, wakuu wa shule za sekondari na walimu wa wakuu wa shule za Msingi halmashauri ya wilaya ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanawasimamia vyema walimu ili kuinua kiwango cha elimu katika halmashauri hiyo.
Mweli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na watendaji hao alipofanya ziara ya siku moja kwenye halmashauri hiyo ambapo pia alikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Mweli, vyumba vya madarasa sekondari ya Nyehunge na ujenzi wa vyumba vinane na matundu 10 ya vyoo vya sekondari mpya ya Sukuma.
Licha ya kupongeza hatua mbalimbali na jitihada za ujenzi wa miundombinu ya madarasa, lakini alisema hawajafanya vizuri katika taaluma hivyo wanatakiwa kubadilika na kuongeza bidii kiutendaji.
Halmashauri hiyo, katika matokeo ya darasa la saba mwka 2020 imekuwa ya mwisho katika halmashauri nane za mkoa wa Mwanza.
“walimu wakuu hawajasimamiwa vyema waliapo, tuna walimu wa kutosha katika masomo ya sanaa lakini ufaulu upo chini bado watoto wanafeli masomo hayo, sasa ninataka alama C ziwe nyingi za masomo ya sanaa hapa,” alisema
Alisema kama kuna walimu ambao wanashindwa kufundisha wakitumia sifa za kuwa wake wa viongozi, wasiwaogope badala yake watoe taarifa kwenye ngazi za juu ili waweze kuondolewa katika maeneo hayo.
“Kuna wale wanajiita wake wa vigogo, inawezekana labda kweli ni mke wa mkurugenzi hafundishi unashindwa kumchukulia hatua, wewe tupeni taarifa sisi tutamwondoa, au piga simu ya call center wala haina haja ya kujitambulisha toa malalamiko yako tutayapata na kuyafanyia kazi,” alisema
Kuhusu motisha, alisema zipo aina mbalimbali za walimu kupewa motisha huku akitolea mfano wa mwalimu wa serikali anapokwenda kusoma bado anaendelea kulipwa mshahara wake na iwapo kama anaishi kwenye nyumba ya serikali inaendelea kuwa yake mpaka amalize masomo.
Lakini akimaliza masomo akarudi shuleni anapandishwa daraja tofauti na ilivyo kwenye sekta binafsi ambapo mfanyakazi akienda kusoma mara nyingi huwa wanasimamishwa kazi hivyo akimaliza anaanza upya kuomba kazi nyingine.
Alisema kwa sasa Serikali ina mpango wa kujenga shule 1,000 nchi nzima ambazo zaidi zitajengwa kwenye kata ambazo hazina shule kabisa au kwenye kata ambazo zina shule lakini zina uhitaji wa shule zingine.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Awali na Msingi, kutoka Tamisemi, Susan Nussu alisema halmashauri hiyo kwa kipindi cha nyuma ilikuwa ikifanya udanganyifu wa mitihani hivyo hawatarajii kuona udanganyifu huo ukiendela kutokea.
Nao baadhi ya watendaji hao walisema shule zao zinafeli kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mrundikano wa watoto, uhaba wa walimu na mwamko wa wazazi kuhusu elimu.
Kwa mwaka 2020 halmashauri hiyo ilisajili wanafunzi 9,981, waliofanya mtihani walikuwa wanafunzi 8674, kati yao walifaulu wanafunzi 6394, sawa na asilimia 73.7, huku walioshindwa ni wanafulu 2,280 sawa na asilimia 26.28.