Home Mchanganyiko MBUNGE KOROGWE VIJIJINI AKERWA NA KASI NDOGO YA UTEKELEZAJI WA MAJI MAZINDE

MBUNGE KOROGWE VIJIJINI AKERWA NA KASI NDOGO YA UTEKELEZAJI WA MAJI MAZINDE

0

………………………………………………………………………………………

Mbunge wa korogwe vijijini Timotheo Mzava akerwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa maji mazinde huku amuru Mkandarasi aliopo aondolewe kwa kushindwa kumaliza kwa wakati mradi huo uliogharimu zaid ya shilingi bil.51 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano

Akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi kwa kukichagua chama cha Mapinduzi CCM na yeye kuwa Mbunge wa jimbo hilo uliofanyika kata ya Mazinde wilayani korogwe

Mbunge huyo alisema mradi huo ungewasaidia wananchi kupata maji safi na salama ulikuwa ukamilike tangu mwaka jana mwezi wa 11 lakini hadi Sasa haujakamilika na wananchi wanaendelea adha ya kukosa maji ya uhakika huku wakiuziwa maji kwa sh? 2200 kwa mwezi.

Mbunge huyo alisema mradi huo unasimamiwa na Wakala wa maji safi na usafi wa Mazingira vijijini (Ruwasa) kasi yake hailizishi hivyo aliwataka viongozi wa chama na Serikali kata kumuita Meneja wa Ruwasa ili awaeleze matumizi ya hizo pesa zaid ya milion 51 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ukarabati wa mradi huo zimefanya kazi gani licha ya muda wa kukabidhi mradi huo umeshapita .

Mkandarasi aliyepewa mradi huo Bakari Mtawazo alisema changamoto kubwa iliyofanya mradi usikamilike kwa wati ni kutokana na ardhi ya Mazinde kuwa na mawe makubwa na mwamba ambao hauchimbiki hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi ambapo alieleza kwa Sasa wameshapata watalaam wanaochoma mawe ili waweze kukamilisha mradi huo hivyo mwezi mmoja tuliopewa tutakuwa tumeshakamilisha.

Alisema mradi huo wa ukarabati ulikuwa ukamilike mwezi wa 11 mwaka jana Kama mkataba ulivoonyesha lakini kulingana na sababu zilizotajwa hapo juu na ikiwemo ya ucheleweshwaji wa fedha ndio imepelekea kutufanya usikamilike kwa wakati.

Mtawazo alifafanua mradi huo unajumla ya mita 1350 na mita ambazo zimechimbwa na kulazwa mabomba ni mita 650 na kwamba mita ambazo ziko tayari ni 400 na mita ambazo bado 300 na hizo zimechelewa sababu kulikuwa na changamoto ya wakulima wa tangawizi ambao walikuwa hawajavuna.

Hata hivyo Mhandisi wamaji kutoka Wakala wa maji safi na usafi wa Mazingira (Ruwasa) Korogwe Joyce Malekela alisema walipokea zaidi ya milion 127 kutoka serikalini kwaajili ya kukarabati wa miradi tisa iliyoathiriwa na mafutiko ikiwemo huu wa Mazinde ambao haujakamilika kutokana na changamoto mbalimbali.

Malekela alisema kuwa kwasasa wamesharekebisha baadhi ya changamoto hivo wamempa mwezi mmoja fundi anayetekeleza mradi huo akamilishe ili wananchi waweze kupata maji ya uhakika na waondokane na changamoto inayowakabiri na tatizo la maji liwe historia.

Mzava ameanza ziara rasmi ya kupita kuwashukuru wananchi kwa kumchagua yeye na chama chake ambapo ameanza na kata ya Mazinde Kama Mgombea urais ambaye kwasasa Ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivopita Mazinde wakati was kampeni alimtaka atakapo anza ziara aanzie kata hiyo ya maazinde.