Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu akizungumza wakati akizindua ugawaji wa hati za viwanja na mashamba zilizotolewa na kampuni ya Choemu Investiment inayojishughilisha na miradi ya kupima viwanja na mashamba na kuuza kwa bei nafuu katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Peter Mayunga Mkurugenzi wa Kampuni ya Choemu Investiment inayojishughulisha na miradi ya kupima viwanja na mashamba na kuuza kwa bei nafuu katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam akizungumza na wateja mbalimbali waliokabidhiwa hati zao leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu akikabidhi hati ya kiwanja kwa Seif Kasingo Mkazi wa Tabata ambaye ni mteja wa kampuni hiyo kulia ni Peter Mayunga Mkurugenzi wa Kampuni ya Choemu Investiment.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu akikabidhi hati ya kiwanja kwa Bestina Mkolokoti mkazi wa Mbezi ambaye ni mmoja wa wateja wa kampuni hiyo kulia ni Peter Mayunga Mkurugenzi wa Kampuni ya Choemu Investiment
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu akimpongeza Peter Mayunga Mkurugenzi wa Kampuni ya Choemu Investiment baada ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja wa kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya picha zikionesha wateja mbalimbali wa kampuni hiyo waliohudhuria katika shughuli hiyo.
KAMPUNI ya uuazaji wa viwanja na mashamba kwa mkopo usio na riba wala dhamana ya Cholemu Investment Limited imepongezwa kwa juhudi inayoonyesha
katika utoaji wa elimu na kuuza viwanja na mashamba kwa kuzingatia sheria za ardhi na mipango Miji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Kazi Maduhu amesema, taarifa za upimaji, upangaji na uuzaji wa ardhi ni muhimu kwa wananchi ili waweze kufanya machaguo sahihi na kuepukana na migogoro ya ardhi.
“Kinachofanywa na Cholemu ni cha kuigwa hasa kwa kutoa taarifa sahihi za ardhi, ukimiliki ardhi wewe sio maskini… sisi kama Manispaa tutahakikisha wananchi wanafikiwa na taarifa sahihi za ardhi pamoja na kutambua haki zao hasa za umiliki wa hati.” Amesema.
Amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakinunua ardhi na kupuuza suala la umiliki wa hati.
“Manispaa ya Kinondoni tuna hati 735 hazijachukuliwa na hii inadhihirisha kuwa watu hawa hawalipi kodi jambo linaloweza kuwapoteza umiliki wa ardhi, wananchi watambue kuwa hii ni haki ya kila mmliki wa ardhi na anachotakiwa ni kuipata, kuitunza na kulipa kodi.” Amesema.
Pia amewapongeza Cholemu Investment Limited kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kupanga, kupima ardhi na kutoa taarifa sahihi kuhusiana na upatikanaji wa ardhi na kuwataka kukutana na kata kumi za Manispaa hiyo na kutoa elimu zaidi pamoja na kuendelea kufuata sheria, taratibu na kuwa waadilifu.
Kwa upande Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Peter Mayunga amesema, wamekuwa wakiuza ardhi kwa wazawa kwa mkopo usio na riba na dhamana pamoja na kutoa hati kwa wateja wao.
“Tumekuwa tukishirikiana na wataalamu wa Manispaa katika upangaji wa Miji kwa kuhakikisha wananchi wanapata ardhi isiyo na migogoro.
Ameeleza kuwa malipo ya viwanja hufanyika kidogo kidogo na kwa awamu na wanapatikana katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Pwani na Dodoma.
Vilevile amesema kuwa, vijana ni nguzo muhimu katika kulipeleleka taifa mbele zaidi kwa kuwekeza katika ardhi.
“Tunaendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapa elimu zaidi hasa ya umuhimu wa kumiliki ardhi na hati….hii ni moja ya changamoto tunayokumbana nayo tuna hati 80 za mashamba ambazo hazijachukuliwa hadi sasa ” amesema.
Semina elekezi hiyo iliyowakutanisha na vijana imekwenda sambamba na utoaji wa hati za umiliki wa ardhi kwa wateja waliohudumiwa na kampuni hiyo.