******************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu Yanga inaendelea kuwa wagumu kupoteza mechi katika ligi baada ya kulazimishwa sare na maafande wa Tanzania Prison katika dimba la Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
Timu zote zilienda mapumziko zikiwa hazijapata kitu na katika kipindi cha pili Tanzania Prison walianza kwa kupata bao kupitia kwa Jumanne Elifadhili mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
Yanga ilionesha kutaka kurudisha bao kwani walionekana kulisakama lango la maafande na kufanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Mshambuliaji wao Saidi Ntibazonkiza mnamo dakika ya 76.