Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza (katikati) akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi wa Kada nyingine hawapo pichani, alipokuwa kwenye kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma mapema leo asubuhi Jijini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa, Askari na Watumishi wa Kada nyingine
***************************************
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Mbaraka Semwanza kwa niaba ya Kamishna Jenerali amewaasa Maafisa na Askari kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na weledi wakati wa kutekeleza majuku yao.
Kamishna Semwanza aliongea hayo kwenye kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu Dodoma cha kufunga mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka mpya 2021 mapema leo asubuhi na kusisitiza nidhamu kwa Watumishi hao.
Hatuwezi kutimiza majuku yetu vizuri kama hatutazingatia sheria na kanuni ambazo zinatutaka muda wote tukiwa kazini na nyumbani kuwa na nidhamu ya hali ya juu, alisema hayo Kamishana Semwanza.
Sinto mvumilia yeyote yule ambaye ataenda kinyume na matwaka ya kiutumishi ambayo yanatutaka kuwa waadilifu tunapotekeleza majukumu yetu, tukumbuke kuwa serikali imetupa dhamana ya kuokoa Maisha ya watu na mali zao Pamoja na jukumu la kukusanya maduhuli ya serikali katika ukaguzi tunaoufanya kwenye majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji.
Aidha Kamishna Semwanza akiendelea kutoa maelekezo kwa Maafisa, Askari na Watumishi wa kada nyingine, ameagiza tunapoelekea kuanza mwaka mpya wa 2021 tuongeze juhudi katika maeneo ya kutoa elimu kwa umma, kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari kwenye majengo yote yakiwemo majengo ya serikali Pamoja na vyombo vya usafiri na usafirishaji vya nchi kavu na majini.
Kamishna Semwanza amewataka Maafisa na Askari kuhakikisha majengo yote yanayojengwa hapa nchini ramani za michoro ya majengo hayo zinafika vituo vya zimamoto na uokoaji na kuzipitia kisha kutoa ushauri wa kitaalum ili kuimarisha usalama wa majengo hayo. Tusikae maofisini twendeni kwenye maeneo hayo kukagua kuona kuwa wameleta ramani hizo vituoni alisema Kamishna Semwanza.
Kamishna semwanza amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwenye Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pale wanapoona majanga ya moto au maokozi kwa kutoa taarifa mapema. Tukipata taarifa mapema itakuwa ni rahisi kukabiliana na janga la moto kabla madhara hayajakuwa makubwa hali kadhalika swala la maokozi. Kuokoa Maisha na mali ni jukumu letu la msingi.