Home Mchanganyiko NAIBU KATIBU MKUU KAILIMA ATEMNELEA VITUO VYA POLISI DAR ES SALAAM LEO.

NAIBU KATIBU MKUU KAILIMA ATEMNELEA VITUO VYA POLISI DAR ES SALAAM LEO.

0

***********************************************

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi, Ramadhani KAILIMA (wapili kulia), leo Disemba 31, 2020, amefanya ziara ya kikazi ya ukaguzi wa baadhi ya vituo vya Polisi jijini Dar es Salaam.

Katika ziara yake hiyo, Kailima ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Malalamiko wa Wizara hiyo, Kamishana wa Polisi (CP), Albert Nyamuhanga.

Ziara ya Kailima ilianza kwa kukutana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kabla ya ukaguzi wa vituo hivyo.

Naibu Katibu Mkuu huyo, alipata maelezo ya uhalifu katika Kanda hiyo na baadaye kukagua vituo vya Polisi hasa Mahabusu ya Vituo vya Mbagala Maturubai (Mkoa wa Kipolisi Temeke), Mburahati na Kituo cha Polisi Kijitonyama (Mkoa wa Kipolisi Kinondoni).

Aidha, Kailima amewashauri Wakuu wa vituo hivyo kupunguza msongamano wa Mahabusu ambao kesi zao zinaweza kupatiwa dhamana