Home Mchanganyiko RC NDIKILO AZIAGIZA HALMASHAURI MKOANI PWANI KUWABANA WATENDAJI AMBAO NI WEZI WA...

RC NDIKILO AZIAGIZA HALMASHAURI MKOANI PWANI KUWABANA WATENDAJI AMBAO NI WEZI WA MAPATO

0

**************************************

MWAMVUA MWINYI,PWANI

29,des
SERIKALI Mkoani Pwani, imeagiza halmashauri zote mkoani hapo kuhakikisha zinadhibiti mianya ya wizi wa mapato na kuwabana watendaji watakaokuwa na uroho wa kuingiza mapato mifukoni mwao.
Aidha imeelekeza, mikataba tata irejewe upya kwani halmashauri zina haki ya kufanya hivyo ili kujiridhisha.
Akifungua kikao cha ushauri mkoani Pwani, Mkuu wa mkoa huo,mhandisi Evarist Ndikilo alisema makusanyo ya mapato ya ndani ya baadhi ya halmashauri hayaridhishi kwani zipo halmashauri zenye asilimia 20-50 ya ukusanyaji wa mapato.
Aliagiza ,kuziba mianya iliyopo ya upotevu wa fedha za mapato na watendaji wachache wanaovujisha mapato wabainike .
“Na kwa hili nipo serious kabisa ,watendaji wababaishaji ,wanaohujumu fedha za serikali wakamatwe,wale wanaotumia posi zao wachunguzwe,watakaobainika kuhusika washtakiwe na wafungwe” alifafanua Ndikilo .
Ndikilo alisema, mabaraza ya madiwani wa halmashauri, yakae kuangalia watendaji wazembe na wezi wasiojali maslahi ya wananchi na wawashughulikie.
Kuhusu TIN Number, alidai kwa wawekezaji na wafanyabiashara ,anashukuru mkoa umemaliza changamoto hiyo ,wengi wao kwasasa wanalipia Pwani.
Mbunge wa jimbo la Rufiji ,Muhammed Mchengerwa àlisema ingekuwa vyema halmashauri zinazopitiwa na bomba la gesi wakafaidika na kodi ya huduma 0.03 asilimia ambayo wangepaswa kuipata.
Pamoja na hayo ,mbunge wa jimbo la Mafia ,Omary Kipanga aliomba zao la Mwani likaingizwa katika taarifa ,kwakuwa ni moja ya zao la kibiashara linalolimwa Mafia kama ilivyo korosho.