Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Isabela Chilumba akicheza Ngoma ya Asili ya Chihoda katika Kilele cha Tamasha la Utalii lililofanyika Nyasa Mkoani Ruvuma Hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba akiwa katika Boti ya Uvuvi akiwa anaelekea Katika Kisiwa cha Lundo kutalii katika Tamasha la Utalii lililofanyika Nyasa Mkoano Ruvuma
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya akiongea na Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii bw Allan Kijazi wakati walipotembelea mabanda ya wanyamapori katika Tamasha la Utalii Nyasa.
***********************************************
Mkuu wa wa Wilaya ya Nyasa amewataka wawekezaji wa Utalii , kuwekeza Wilaya ya Nyasa kwa kuwa Wilaya ya Nyasa ina Vivutio Vingi vya Utalii ambavyo, ni Vya kipekee ambavyo Vinapatikana Wilaya ya Nyasa pekee .
Ameyasema hayo jana, , wakati akihutubia wananchi alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Cristina Mndeme katika Kilele cha Tamasha la Utalii 2020, lililofanyika katika Viwanja vya fisheries, Mbamba bay Wilayani Nyasa.
Mkuu huyo alifafanua kuwa Wilaya ya Nyasa ni Wilaya, ya kipekee katika Mkoa wa Ruvuma, ambayo ukishindanisha na Wilaya zingine za Mkoa wa Ruvuma, ina Vivutio vingi vizuri vinavyowavutia wageni wengi, hasa Ziwa Nyasa na Fukwe zake za Asili ambazo zimeifanya Wilaya, hii kuwa ni ya kipekee, na kuwataka wawekezaji kuja kuwekeza Wilaya ya Nyasa.
Aliongeza kuwa Wilaya ya Nyasa pia ina miundombinu rafiki, ya kuwavutia watalii na Wawekezaji ukizingatia kuwa Barabara ya Mbinga hadi Mbamba bay, Tayari imekamilika na Hospitali ya Wilaya ya Nyasa imeanza Kazi na kutoa huduma kwa, wananchi na kuwawafanya hata watalii na wawekezaji hata wakiumwa watatibiwa na kupata huduma bora za kiafya.
Aidha kwa upande wa usafiri wa Maji, amewatangazia wananchi kuwa Usafiri wa Meli ya Kisasa ya Mizigo ya Mv Mbeya 11 inaanza rasmi kazi na jumanne wiki hii itatia Nanga katika Bandari ya Mbamba bay, na Meli ya Mv Njombe nayo inafanya kazi.
Aidha amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa Juhudi zake za kuiboresha Wilaya ya Nyasa, hasa kwa miundombinu Wilaya ya Nyasa, na sasa Hakika ni Wilaya ya Kitalii.
“Nichukue Fursa hii kumpongeza sana Mh Rais, kwa Juhudi zake alizozifanya hasa kwa upande wa miundombinu, ametujengea barabara ya Lami na kwa kwa sasa inapitika mwa haraka na muda wote tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Upande wa Usafiri wa majini Meli kubwa mbili zinafanya kazi na Mv Mbeya imeanza kazi rasmi na Jumanne itawasili Mbamba bay hivyo, Mbamba bay imefunguka nawakaribisha sana wawekezaji”.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ambaye pia ni Kamishna wa Uhifadhi Tanzania National parks TANAPA, Mh. Allan Kijazi amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuandaa Tamasha la Utalii kwa miaka mine mfululizo, na kuwashauri kuwa wanatakiwa kuwa na Siku maalum na Tarehe maalumu ya kutangaza Vivutio vyot, na Wizara ya Maliasili na Utalii imeyapokea maombi ya kuchangia na kuandaa Tamasha lenye Hadhi ya Kimataifa.
Naye Mbunge Wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, ameliomba Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, kupitia Safari Channel Kuja kutengeneza makala na Vipindi mbalimbali vya Vivutio vya Wilaya ya Nyasa, ambavyo ni vya aina yake kwa kuwa vivutio vingi vya wanyama watanzania wanavifahamu sasa ni zamu ya kutangaza Ziwa Nyasa na Fukwe zake.
Tamasha hili limepambwa na Ngoma za Asili za Chioda, Muhambo na Lingoga, mashindano ya kuogelea, kupiga kasia na Utalii wa Kisiwa Cha Lundo pamoja na Utali wa Nyama choma.