Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Kenneth Hosea akizungumza katika mkutano mkuu wa TAHLISO uliofanyika jijini Dar es salaam na kujadili mambo mbalimbali kuhusu Chamamoto zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya vyuo vikuu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO Bw. Peter Niboye akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye Chuo cha Ustawi wa jamii jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC),Bw. Yessaya Mwakifulefule akitoa salamu zake kutoka shirika hilo katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali za vyuo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Kenneth Hosea kushoto na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO Bw. Peter Niboye wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya maofisa mbaalimbali kutoka taasisi za serkali walioshiriki katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC),Bw. Yessaya Mwakifulefule kushoto na Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF, Bw Christopher Mapunda wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Kenneth Hosea kushoto Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO Bw. Peter Niboye pamoja na viongozi wengine wa TAHLISO wakishiriki kuimba wimbo wa taifa.
…………………………………………..
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC),Bw. Yessaya Mwakifulefule amesema shirika hilo limeamua kudhamini mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO) ili waweze kujadiliana pia kuelimishana kuhusu umuhimu wa kujiunga na bima ili kuepuka majanga yanayoweza kuwapata wakiwa vyuoni wakiendelea na masomo.
“Tunaamini kuwa wanafunzi hawa wanapomaliza vyuo wanaenda kuwa viongozi na maafisa katika mashirika na taasisi mbalimbali. Wakiondoka na elimu ya bima wakiwa mashuleni itakuwa ni rahisi pia kuwashawishi na wengine kujiunga,” amesema Mwakifulefule.
Aliongeza pia, kuwa lengo la kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anajiunga na bima ili kulinda maisha na usalama wa mali zake awapo shuleni
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa (TAHLISO) Bw. Peter Niboye amesema idadi kubwa ya wanafunzi wanaofaidika na mkopo wanalalamika juu ya kupunguzwa kwa fedha za malazi ambazo zilisababishwa na changamoto za mfumo wa elektroniki.
“(TAHLISO) inaomba serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuboresha mifumo ya kielektroniki ili kuepuka kero zinazowapata wanafunzi wakati wa malipo na ufuatiliaji,” amesema.
Akijibu hoja za wanafunzi Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Kenneth Hosea amesema serikali kwa sasa inaimarisha na kuboresha mifumo ya mawasiliano ili kutatua changamoto hizo.
Amesema serikali inaendelea kutatua changamoto hizo kupitia wizara na taasisi zinazohusika na masuala ya wanafunzi wa elimu ya juu.
“Mfumo wa ufadhili utaboreshwa ili kusiwepo na mwanafunzi atakayepata kidogo au zaidi kwa kile anachotakiwa kupata katika mkopo wake. Utusamehe sisi (serikali) kwa kile kilichotokea hapo awali, ”alisema.
Dk Hosea ameongeza kuwa serikali imepanga kuongeza pesa ili kutoa mikopo kwa wanafunzi zaidi katika siku zijazo.
“Tunapanga kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka 157, 770 waliosajiliwa katika mwaka wa masomo wa 2020/2021. Kwa kuzingatia hilo, tunataka pia idadi ya wanufaika wa mkopo kuongezeka,”alibainisha.
Kwa sasa wanufaika wa mkopo waliongezeka hadi 145, 000 katika mwaka wa masomo 2020/21, wakitoa Sh464 bilioni, kutoka 132, 119 zilizorekodiwa mwaka jana na mkopo huo wenye thamani ya Sh450 bilioni.
Mkutano huo uliwakutanisha maraisi wa vyuo vikuu na mawaziri wao wa afya na mikopo pamoja na maafisa wa serikali ili kujadiliana kujadiliana kutokana na changamoto za kupungua kwa mikopo ya wanafunzi kutokana na hitilafu za kimtandao katika mfumo wa malipo ya fedha za mikopo zilizowasilishwa kwenye mkutano huo na uelewa mdogo wa wanafunzi juu ya mfumo mpya wa uandikishaji na malipo wa Shirika la Bima la Afya (NHIF).