NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Marry Prisca Mahundi kulia akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea eneo la Kilapura ambalo limejengwa tenki kubwa la kuhifadhi maji katika mradi unaotoa maji eneo la Pongwe kupeleka wilayani Muheza wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly |
NAIBU
Waziri
wa Maji Mhandisi Marry Prisca Mahundi kulia akitoka kwenye mradi wa maji
unaotoa maji eneo Kilapula Pongwe Jijini Tanga unaopelekea wilayani
Muheza mara
baada ya kutembelea eneo la Kilapura ambako pia kumejengwa tenki kubwa
la
kuhifadhi maji wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga wa kwanza na katikati
ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo na wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na wa tatu
kutoka kushoto ni Mhandisi Salum Hamisi kutoka Tanga Uwasa
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Marry Prisca Mahundi katikati akimsikiliza kwa umakini Mhandisi Salum Hamisi kutoka Tanga Uwasa akimueleza namna mitambo ya kusafishia maji kwenye kituo cha Mowe Jijini Tanga inavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya kikazi kulia ni Meneja Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani katikati aliyevaa shati jekundu ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Marry Prisca Mahundi amewataka wananchi wanaopita kwenye bwawa kwenye bwawa la mabayani ambalo ndio chanzo kikuu cha maji kutoka kwenye mapori kwa shughuli za kibinadamu waache mara moja kwani wanahatarisha maisha yao lakini pia wanasababisha uchafuzi wa mazingira.
Mhandisi Marry Prisca alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga aliyoianzia kwenye kukagua shughuli za ujenzi wa mradi wa Maji Pongwe Muheza unaotekelezwa na Tanga Uwasa kwa gharama ya kiasi cha Bilioni 6.1 na kituo cha kusafishia Maji eneo la Mowe.
Alisema ni vema wananchi hao kuacha kufanya hivyo katika bwawa hilo ambalo ndio chanzo kinacholisha maji kwa zaidi ya asilimia 90 kwa wananchi na halijawahi kukauka wala kupungua kina chake.
Huku akionyesha kuridhishwa na juhudi ambazo zimefanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) kwa kushirikiana kudhibiti shughuli za kibinadamu kwa mita 500 kutoka kwenye bwawa la Maji cha Mabayani.
Amesema hatua hiyo imepelekea bwawa hilo ambalo ndio chanzo kikuu cha Maji kwa wakazi wa Mji wa Tanga na maeneo mengine limetunza na kuwa na hivyo kupelekea upatikanaji wa maji katika mji wa Tanga kuendelea kuwa ya uhakika kutokana udhibiti.
“Katika hili niwapongeza Tanga Uwasa na Ruwasa kwa kuweza kushirikiana kwa pamoja kuona chanzo hicho kinaendele kuwa cha manufaa makubwa na kuona usambazaji wa maji unaendelea kuongezeka mitandao ya kusambaza maji mji wa Tanga umeendelea kuboresha”Alisema
Naibu Waziri huyo alisema kwani hatua hiyo imewezesha kuongeza chanzo kingine kikubwa ambacho kitaendelea kupunguza tatizo la mgao wa maji na tunatarajia baada ya miezi miwili tatizo la mgao wa maji wilayani Muheza linakwenda kumalizwa kwa maana maji hayatakuwa yakitolewa kwa mgao.
“Lakini niwasihi watendaji wa Ruwasa na Tanga Uwasa tuendelee kushirikiana kila mmoja aweza kutimiza wajibu wake kama ni Ruwasa hakikisha waliopo pembezoni mwa miji mikubwa wanaendelea kupata huduma ya maji kwa walipo katikati tunafahamu wanapata maji ya kutosha huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutunzwa kwa mazingira kwenye vyanzo vya maji “Alisema
Akiwa kwenye mradi unaotoa maji kutoka Pongwe kwenda Muheza eneo la Kilapula, Naibu Waziri huyo aliwahakikishia wananchi wa mji wa Muheza kwamba ambao kwa sasa wanakabiliwa na adha ya mgao wa maji kuwa mradi huo wa Pongwe –Muheza utakamilika mwezi February mwakani.
Alisema kwa sababu Serikali imeamua kumlipa mkandarasi fedha zake zote mapema mwezi Januari 2021 ili asiwe na sababu yoyote ya kuchelewesha mradoi huo.
Mradi huo ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimia 80 umejengwa kwa awamu tatu kwa kuhusisha ujenzi wa pampu na tenki la kuhifadhi maji katika eneo la kilapula.
Aidha pia shughuli nyengine ambazo zimefanyika ni ulazaji wa bomba kubwa kutoka Pongwe hadi katika mitambo ya kusafishia maji Mowe ili kuwezesha wananchi wa Muheza kupata maji kwa saa 24 badala ya mgao wa siku tatu kwa wiki unaofanyika hivi sasa.
Awali akizungumza wakati Naibu Waziri huyu alipokuwepo kwenye chanzo cha Maji katika Bwawa la Mabayani, Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema changamoto kubwa ilikuwa ni uvamizi na wananchi kufanya shughuli mbalimbali na wananchi kufanya kama njia ya kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwengine.
Alisema kumeshatokea ajali watu wamekufa kutokana na mvua zinapokuwa nyingi maji yanapokuwa mengi kwenye bwawa hilo watu wanadumbukia na wameweka ulinzi na wanajitahidi kulinda kuzuia watu wasipite japo changamoto kutokana na watu wengine kutokea maporini.
Mkurugenzi huyo alisema lakini kwa hali ilivyo wamejitahidi kutunza mazingira huku akieleza sehemu kubwa ya uvamizi imepungua na wanashirikiana na kamati za vijiji kwenye maeneo hayo kutunza mazingira wenyewe kwa wenyewe wanalindani na hata miti haikatwi kwa sasa.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo ,Mkuu wa kitengo cha Uzalishaji Maji wa Tanga Uwasa Mhandisi Joseph Mkuki alisema kwamba bwawa hilo la mabayani lilijengwqa mwaka 1976 na kumalika 1978 na ndio chanzo kikubwa cha maji kwenye Jiji la Tanga.
Alisema bwawa hilo linauwezo wa kuhifadhi maji mita za ujazo milioni 7.7 na linapokea maji kutoka Mto Zigi chanzo chake kikiwa ni Milima ya Usambaza na Amani Muheza na linaweza kutosheleza mahitaji ya maji kwa Jiji la Tanga miaka kadha ijayo kabla ya kufanyika upanuzi.
Alisema upanuzi huo utafanyika kutokana na uwepo wa miradi mikubwa kwa miaka ya baadae ikiwemo ongezeko la wakazi wa Jiji la Tanga limeongezeka na vilevile eneo la kutolea huduma kwao limeongezeka ukijumlisha wilaya za Muheza na Pangani.