Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wadau wa mifumo ya kuuza maudhui na kazi za Sanaa kwa njia ya mtandao, lengo likiwa ni kutafuta mifumo mizuri yenye ubora na viwango itakayosadia wasanii kuuza kazi zao. Kikao hicho kimefanyika Desemba 17, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Bw.Ande John kutoka Clouds Media akizungumza katika kikao cha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na wadau wa mifumo ya kuuza maudhui na kazi za Sanaa kwa njia ya mtandao, lengo likiwa ni kutafuta mifumo mizuri yenye ubora na viwango itakayosadia wasanii kuuza kazi zao. Kikao hicho kimefanyika Desemba 17, 2020 Jijini Dar es Salaam. Bw. Lumuliko Mengele akitoa maoni katika katika kikao cha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na wadau wa mifumo ya kuuza maudhui na kazi za Sanaa kwa njia ya mtandao, lengo likiwa ni kutafuta mifumo mizuri yenye ubora na viwango itakayosadia wasanii kuuza kazi zao. Kikao hicho kimefanyika Desemba 17, 2020 Jijini Dar es Salaam.
*************************************
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa Serikali katika kukuza na kuhakikisha maslahi ya wasanii yanaboreshwa, imeanza kupokea mawazo kuhusu namna bora ya kutumia mifumo ya kiteknolojia katika kuuza kazi za Sanaa
Dkt. Abbasi ameyasema hayo Desemba 17, 2020 Jijini Dar es Salaam alipokuatana na kufanya kikao na wadau wa mifumo ya kuuza kazi za Sanaa ambapo amesema kuwa Serikali inataka kuweka mazingira bora ya kufanya kazi ya Sanaa ambayo itawanufaisha na kuwasaidia kupata soko la uhakika huku akisistiza kuwa mifumo ambayo wadau watapendekeza lazima iwe bora katika kuonyesha maudhui na yenye viwango bora.
“Wasanii mnapaswa kutumia teknolojia ambayo kwa sasa ndio inabeba soko la kuuza n kazi zenu, na lazima mtambue kuwa “teknolojia huwezi kushindana nayo ila unaweza kufaidika nayo” hivyo ni jukumu lenu kutumia fursa hiyo”,alisema Dkt.Abbasi.
Aidha, Dkt. Abbasi amewataka wabunifu na wasanii wote kusajili kazi zao katika Taasisi ya Hakimili Tanzania (COSOTA) ili zilindwe na Sheria ambazo zinasimamiwa na Serikali lengo likiwa ni kuwanufaisha wasanii hao.
Vilevile, Dkt. Abbasi amewaagiza wasanii hao na wadau wote wa Sanaa kuwasilisha serikalini tozo zote ambazo zimekuwa ni kero katika kutekeleza kazi zao ifikapo Desemba 31, 2020 ili Serikali izifanyie kazi.
Naye Bw. Lumuliko Mengele kutoka Kampuni ya Blackball ameishukuru Serikali kuona umuhimu wa kutumia mifumo katika kuuza kazi za Sanaa ambapo ameshauri kuwa mifumo hiyo iwe na uwanja mpana katika kufanya kazi hiyo.
Kwa upande wake Bw.Emmanuel Godfrey ameshauri kuwa mifumo itakayoridhiwa lazima iwekewe vigezo ambayo watumiaji wengi watakuwa na uwezo wa kuvifikia huku akisistiza kuwa Serikali iiratibu mifumo hiyo.