Mkurugenzi wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa BANDO TAM TAM PLUS pamoja na huduma mpya ya vifurushi ya JISOTI iliyofanyika kwenye duka la huduma za TTCL Corporation lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Corporation, Bw. Vedastus Mwita pamoja na Meneja Bidhaa wa TTCL, Bw. John Yahya.
Mkurugenzi wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Corporation, Bw. Vedastus Mwita (wa pili kushoto) kwa pamoja wakivuta utepe kuashiria uzinduzi wa BANDO TAM TAM PLUS pamoja na huduma mpya ya vifurushi ya JISOTI iliyofanyika kwenye duka la huduma za TTCL Corporation lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Corporation, Bw. Vedastus Mwita (wa pili kushoto) kwa pamoja wakivuta utepe kuashiria uzinduzi wa huduma mpya ya vifurushi ya JISOTI iliyofanyika kwenye duka la huduma za TTCL Corporation lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Corporation, Bw. Vedastus Mwita akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa BANDO TAM TAM PLUS pamoja na huduma mpya ya vifurushi ya JISOTI iliyofanyika kwenye duka la huduma za TTCL Corporation lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde pamoja na Meneja Bidhaa wa TTCL, Bw. John Yahya wakishuhudia.
…………………………………………
Hadi sasa, T PESA ambayo ni Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, inazidi kuongeza wateja wake siku hadi siku pamoja na Mawakala ambao kwa sasa ni zaidi ya milioni moja na miamala ya takribani Tsh bilioni tano za Kitanzania. Hakika tupo vizuri na Nyumbani ni salama na kunazidi Kunoga.
Kukua kwa T-PESA kumeleta ufanisi na kuongezeka kwa matumizi ya miamala ya kielektroniki ambayo ni pamoja na uuzaji na ununuzi wa bidhaa na utoaji wa huduma kwa njia za kielektroniki kama vile kutuma na kupokea pesa, kulipia ankara za maji, umeme, ada, leseni za magari na usajili wa makampuni huku tukizingatia usalama na unafuu wa huduma zetu.
Aidha huduma hizi zinazidi kutoa fursa ya ajira kwa Wananchi kuwa Mawakala na imekuwa kiungo muhimu cha kurahisisha shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na biashara hivyo ni wito wetu kwamba wananchi waendelee kurudi nyumbani kwakutumia huduma hii ya kifedha yenye manufaa makubwa kwao na Taifa kwa ujumla.
Kutokana na ukweli huu Napenda kuitambulisha kwenu bando jipya ambalo linajulikana kwa jina la Bando Tam Tam Plus, hiki ni kifurushi kilichoandaliwa na TTCL kupitia menu yetu ya T-PESA ambacho kitawawezesha wateja wetu kupata dakika paoja na data kwa bei nafuu Zaidi kuliko kawaida.
Ofa hii tayari iko hewani kuanzia leo ambapo tumeizindua na itadumu sokoni ndani ya kipindi cha miezi mitatu. Kupitia ofa hii Mteja wetu anaweza kujiunga na kifurushi cha siku, wiki au mwezi na akajipatia dakika, sata pamoja na muda wa maongezi kibao kwa gharama nafuu sana.
Hii tumelenga kuwapatia unafuu wa gharama wateja wetu lakini pia ni zawadi yetu ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya kwani wateja wetu wametuunga mkono katika biashara zetu kupitia huduma mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea fedha kupitia simu ya mkononi.
Huduma hii inawalenga wateja wa T-PESA pekee na itadumu sokoni kwa kipindi cha miezi mitatu. Ni Imani yetu kwamba itatoa mchango chanya ikiwemo ongezeko la idadi ya wateja wapya, Mawakala na ongezeko la mapato.
Ili kupata ofa hii, Mteja wa T-PESA atapiga *150*71# kisha atachagua namba 3 na baada ya hapo atafuata maelekezo ili kupata kifurushi anachokihitaji kulingana na fedha na mahitaji yake.
Ofa hii ni sababu nyingine ya wateja wetu kuendelea kutumia huduma zetu kwani kwa shilingi 500 mteja atapata MB 500, dakika 5 kupiga mitandao yote na sms 50 kwa siku, pia kwa shilingi 1000 atapata 1GB dakika 5 mitandao yote, sms 100kwa wiki na shilingi 5000atapata 2 GB, dakika 20 mitandao yote na sms 300 kwa mwezi.
Kulingana na ubora wa ofa hii ni matarajio yetu kwamba itakuwa chachu ya kuongeza mawakala, watumiaji wapya wa T-PESA wapatao 35,000 na kutengeneza faida kwa asilimia 15 ndani ya kipindi cha miezi mitatu ijayo tangu kuzinduliwa kwa ofa hii.
Natoa wito kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Kampuni ya T-PESA za kununua vifurushi, muda wa maongezi, kulipa bili na kufanya miamala mbalimbali ya kifedha .
Nawashukuru wateja wote wa TTCL Corporation na kampuni yake tanzu ya T-PESA na nawakumbusha kua msimu huu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya, kampuni ya T-PESA inazo huduma nzuri na za kipekee huku ikizingatia ubora wa huduma na usala wa fedha za wateja wake.
Aidha niendelee kuwasihi Wateja wetu kuwa makini na matapeli wa kimtandao na niwakumbushe kutunza nambari za siri za matumzi ya mfumo wa T-PESA ili kujihepusha na madhara yanayoweza kutokea kutokana na utunzaji mbaya.