Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, wa pili, akitoka kukagua eneo la Mgodi wa Mlima Igae Suguta unaomilikiwa na kikundi cha Wachimbaji Wadogo wa Hapa Kazi Tu, wilayani Kongwa.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akitoa maelekezo kwa Wachimbaji Wadogo kwenye mgodi wa Mlima Igae Suguta wilayani Kongwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dkt. Selemani Serera kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya mara baada ya mazungumzo kuhusu mgogoro wa Wachimbaji Wadogo wa Mlima Igae uliyopo wilayani humo.
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya, akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo.
*************************************
Na, Issa Mtuwa, Kongwa
Mgogoro wa kugombania shimo la Madini eneo la Mlima Igae katika Kijiji cha Suguta Wilaya ya Kongwa jijini Dodoma lenye leseni namba PML 0193DOM inayomilikiwa na kikundi cha Hapa Kazi Tu, umetatuliwa.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mgogoro huo kutatuliwa na hali ya vuta nikuvute, hivyo kupelekea hali ya uvunjaji wa amani baina ya Colyn Mallya, Kimaro, na Kikundi cha Hapa Kazi Tu wote wakitaka kuchimba bila utaratibu na kupelekea kutokuelewana.
Utatuzi huo, umefanyika jana Disemba 15, 2020, mara baada ya ziara ya Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kutembelea eneo la mgodi wa Mlima Igae.
Kabla kutatua mgogoro huo, Naibu Waziri alitoa nafasi ya kuwasikiliza kila upande wa mgogoro huo ili kupata picha kamili.
Aidha, baada ya kuwasikiza, Mgogoro huo ulitatuliwa kwa kutoa haki kwa wote, wachimbaji na wafadhili, Colyn Mallya ambae amepewe kuchimba miezi mitatu, kisha atapewa Kimaro miezi mitatu baada ya hapo ataachia mgodi kwa kikundi cha Hapa Kazi Tu waendeleze uchimba.
Kwa upande wake, Colyn Malya alisema amekubaliana na maamuzi hayo ili aendelee kuchimba kwa mujibu wa makubaliano, huku mwakili wa Kimaro akikubiana na maamuzi hayo uli uchimbaji uwe na amani.
Wakati huo huo, Yusto Chalo ambae ni mwenyekiti wa Kikundi cha Hapa Kazi Tu, alikubali kwa niaba ya wanachama wake namna alivyotatua mgogoro huo.
Alisema, Naibu Waziri amezingatia maslai ya kila mtu na kwamba wote huwa tunategemea.
“Huu utatuzi nimeupenda, kila mtu amepewa haki na lazima kia mtu aridhike, na umeona kila mtu yuko sawa kama ikitokea mtu akabadilika huyo atakuwa ana jambao lake”, alisema Yusto.
Akitoa taarifa mbele ya Naibu Waziri katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Afisa Madini Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Nachagwa Marwa, alisema baadhi ya Mgogoro iliyopo imeibuka mara baada wamiliki wa leseni Kikundi cha Hapa Kazi Tu, wakilalamika baaddhi ya wafadhili wamekuwa wakifanya kazi za uchimbaji kwenye eneo hilo kwa kuwalubuni baadhi ya wanachama wa kikundi bila kuushirikisha uongoziwa Kikundi.
Akihitimisha mazungumzo na Wachimbaji wadogo, Naibu Waziri amesisitiza juu ya ulipaji wa tozo za Serikali na uuzwaji wa madini kwenye masoko rasmi. Alisema Utoroshwaji wa madini ukikamatwa nayo ni tatizo utajipa umasikini mara baada ya kukamatwa madini.