*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga imezidi kupaa kileleni mwa ligi Kuu Vodacom baada ya kufanikiwa kuizamisha Mwadui Fc mabao 5-0 kwenye dimba la CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Yanga ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Kiungo Mshambuliaji Deus Kaseke ambaye kwa mechi za hivi karibuni amekuwa mwiba kwa timu pinzani.
Magoli mengine ya Yanga yalifungwa na Yacouba 14,49, Kisinda 57 na Lamine 70 na kukamilisha ubao kwa magoli 5-0.