
Mchezaji Isiaka Daudi kutoka Lugalo akijiandaa kupiga Mpira Mbele ya Wachezaji wenzie wakati wa Mashindano ya Golf ya Tanzania Open yanayoendelea TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wachezaji Wanawake walioshiriki wakati wa Mashindano ya Golf ya Tanzania Open wakiwa katika Picha ya Pamoja muda mchache kabla ya kuanza Mashindano yanayoendelea TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mchezaji wa Kulipwa Nuru Mollel kutoka Arusha (kulia) akipiga Mpira Mbele ya Wachezaji wenzie Elisante Lebris(katikati)na Frank Mwinuka (kushoto) wakatia wa Mashindano ya Golf ya Tanzania Open yanayoendelea TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro Nuru ameibuka .
**************************************
Wachezaji wa Golf kutoka Arusha Revinder Singht na Nuru Mollel watamba siku ya Pili ya mashindano ya Wazi ya Golf ya Tanzania yanayoendelea kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Revinder katika siku ya Kwanza ya Mchezo alishika nafasi ya tatu kwa mikwaju ya Jumla 146 nyuma ya George Sembi aliyepiga Mikwaju ya Jumla 145 na Elisha Fadhilili wote wa TPC.
Revinder anaenda hatua ya Tatu baada ya Siku ya pili kupiga Mikwaju ya Jumla 72 na kuongoza huku akifuatiwa na George Sembi wa TPC kwa Mikwaju ya Jumla 76 na Watatu ni Ally Mcharo aliyepiga Mikwaju ya Jumla 77.
Kwa upande wa Wachezaji wa Kulipwa Mchezaji Nuru Mollel ameibuka na Ushindi wa Mashindano haya kwa wachezaji wa kulipwa.
Siku ya Kwanza raundi ya Kwanza Nuru alipata Mikwaju 77 ya pili 71 na siku ya pili Mikwaju 75 na siku ya Mwisho ya Leo Jumamosi amepiga mikwaju 71 huku akifuatiwa na Elsante Lembris wa Arusha na Watatu ni Frank Mwinuka wa Lugalo.
Akizungumzia Mashindano hayo Mwenyekiti wa Chama cha golf cha Wanawake Tanzania TLGU Sophia Viggo ameipongeza TGU kwa kuawapa nafasi Wanawake ambao hawakuwa na nafasi ya kucheza kwa Mujibu wa Katiba.
Wachezaji hao Wanawake wakiwemo Nyota Madina Iddi, Angel Eaton na Neema Ulomi ni Miongoni mwa Wachezaji wanaotupa Karata yao.
Katika Mashindano hayo yanayofanyika katikati ya Mashamba ya miwa katika Kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro yanatarajiwa kufika tamati Jumapili Tarehe 13.