Mapingamizi hayo yametupwa na Jaji A.Z. Mgeyekwa wa Mahakama Kuu anayesikiliza kesi hiyo ya maombi ya mapitio namba 2 ya 2020 yanatokana na rufaa namba 30/2020 iliyokatwa na Bodi ya Thaqaafa.
Kabla ya kutuyatupilia mbali mapingamizi hayo,Wakili wa wajibu maombi Wilbard Kilenzi,akiwasilisha mapingamizi dhidi ya waleta maombi akipinga kuwa Abdallah Amin Abdallah,hana Locus(sehemu)ya kuwa Katibu wa Bodi ya msikiti wa Ijumaa.
Pia kiapo chake kilichopo mahakamani kililetwa bila idhini ya mahakama hivyo hakina mashiko ya kisheria na kuiomba itupilie mbali maombi ya waleta maombi kwa gharama.
Hata hivyo, Wakili wa waleta maombi Godfrey Samson wa LZone Allied Advocate akisaidiwa na Msafiri Henga, waliiomba mahakama kuyatupa mapingamizi ya wajibu maombi kwa gharama sababu hayakutastahili kuletwa kwa misingi ya kisheria.
Jaji Mgeyekwa alikubaliana na hoja ya mawakili wa waleta maombi dhidi ya Bodi ya Thaqaafa ambapo aliendelea kusikiliza na maombi ya mapitio ya rufaa namba 30/2020 yaliyofunguliwa na Bodi ya Msikiti wa Ijumaa kisha akahairisha kesi hiyo hadi Disemba 14, mwaka huu atakapotoa uamuzi.
Rufaa hiyo Bodi ya Thaqaafa ilifungua kesi namba 11/2019 kwenye Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana ikipinga kulipa kodi ya pango sh. milioni 58 kwa mujibu wa mkataba wa upangaji kwenye Zahanati ya Msikiti wa Ijumaa Machi, 2015, wakidai licha ya kuwa ni wapangaji hawastahili kulipa.
Mahakama hiyo chini ya Hakimu Gwaye Sumaye alitoa uamuzi ikiitaka bodi hiyo kuheshimu mkataba wa upangaji wa 2015 ambapo Bodi ya Msikiti ilikaza baada kushinda kesi.
Hata hivyo, Mei 30, 2020 Bodi ya Thaqaafa ilikata rufaa namba 30 ya 2020 kwenye Mahakama Kuu Mwanza,shauri ambalo liliendeshwa hadi Septemba 16,2020 na kutolewa hukumu dhidi ya Bodi ya Msikiti wa Ijumaa.