RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakati hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 8/12/2020.(Picha na Ikulu)
………………………………………..
Makamo wa kwanza wa Rais mteule Maalim Seif Sharif Hamad aliyeapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi ametakiwa kufanya kazi kwa dhati na kukiheshimu kiti cha Rais.
Ikiwa kiongozi huyo ameingia kwenye suk kwa lengo la kushindana na Rais ili aje kumtoa madarakani katika Uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025 maelewano tarajiwa yatapwaya.
Ushauri huo umetolewa Balozi Mstaafu Ali Abeid Karume mara baada ya Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kumuapisha huko ikulu na kuwa rasmi Makamo wake wa kwanza wa Rais.
Balozi Karume amesema licha ya Maalim Seif ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu, anapaswa kukiheshimu kiti cha Rais kwani Dk Mwinyi ndiye mwenye urais.
Ameitaja kazi ya Maalim Seif kwa mujibu wa katiba ya zanzibar ya mwaka 1984 ni kumshauri Rais na kutekeleza majukumu yote atakayopangiwa na Rais.
Balozi Karume amesema ukongwe wa Maalim Seif katika medani za siasa na utawala kisiwe kigezo cha kumfanya adhani yuko sawa na Rais au Rais atapokea maelekezo kutoka kwake.
Amesema badala yake kazi alionayo ni ya ushauri kwa Rais hivyo Rais atakuwa na hiari ya kukubali ushauri huo au kuukataa.
Aidha Balozi amsema ikiwa kiongozi huyo wa upinzani kwa dhati yake aheshimu matakwa ya Rais kisera, kimalengo na kimajukumu anaamini kazi ya kujenga nchi itafanyika kwa umakini.
Mtoto huyo wa pili wa Rais wa Kwanza Zanzibar hayati Mzee Abeid Amanj Karume ,amesema kila mwanasiasa ajue urais haupatikani kwa njama au kwa mizengwe.
Badala yake amesema urais humfika yeyote kwa kudra, bahati na uweza wa mungu wala si kwa hujuma au kwa makeke.
Mwadiplomasia huyo amekitaja chanzo cha mvutano katika suk awamu ya saba amedai kulikuwa na hali ya kutoelewana kati ya Rais na Makamo wake wa kwanza wa Rais.
Amesema jambo la kusikitisha baadhi ya siri za SMZ zikizagaa mitaani kabla hata ya vikao vya BLM havijamalizika Ikulu.
Amemtaja Maalim Seif kuwa ndiye aliyeanza kumtupia vijembe Rais kwenye mikutano ya hadhara , Rais alipoona mambo yanazidi akamjibu na hapo ndio ufa ulipojitokeza.
Amesema hadi wanakwenda katika Uchaguzi mwaka 2015 maelewano yao yalishatetereka hivyo akasema hategemei kama hali hiyo itajirudia tena.