Meneja Mwandamizi wa Mipango Mikakati wa Tanesco, Eng. Costa Rubagumya akitiliana saini mkataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kampuni ya Lung’ali Natural Resources, Father Luciano Mpoma inayoendesha mradi wa Maguta Hydropower 1.2MW umeme unaozalishwa kutoka maporomoko ya maji ya Mto Lukosi, wilayani Kilolo. Tukio hilo limefanyika Makao Makuu ya Tanesco Desemba 8, 2020. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Meneja Mwandamizi wa Mipango Mikakati wa Tanesco, Eng. Costa Rubagumya akishuhudia viongozi wa kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd wakitia saini mkataba kuendesha mradi wa Ijangala Hydropower unaozalisha umeme wa maji kutoka maporomoko ya Mto Ijangala, wilayani Makate yenye uwezo wa kuzalisha 0.36MW.
viongozi wa Kampuni ya Madope Hydro Company Ltd, wakitia saini mkataba wa kuendesha Mradi wa umeme wa Madope Hydropower 1.7MW, unaotokana na maporomoko ya maji ya Mto Madope wilayani Ludewa, Mkoa wa Njombe. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa Mipango Mikakati wa Tanesco, Eng. Costa Rubagumya. Kampuni hiyo itaiuzia umeme Tanesco.
Nicholas Richardson Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SSI Eenergy Tanzania Ltd akisaini mkataba wa kuendesha Mradi wa Kahama Solar Power 10.0MW utakaozalisha umeme wa jua karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama. Miradi yote sita ina uwezo wa kuzalisha megawati 19.16 zitakazouziwa Tanesco.
Viongozi wa Tanesco wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni sita baada ya kutiliana saini mkataba wa kuzalisha umeme na kuiuzia Tanesco. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Tanesco jijini Dodoma .
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma
KAMPUNI sita zimeingia zimesainiana mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa kuziana umeme wa miradi midogo ya kuzalisha umeme.
Tukio hilo limefanyika leo Desemba 8, 2020 katika makao makuu ya Tanesco jijini Dodoma ambapo kampuni hizo zitazalisha umeme wa maji na wa jua.
Kwa upande wa Tanesco mikataba hiyo ilisainiwa na Meneja Mwandamizi wa Mipango Mikakati wa Tanesco, Eng. Costa Rubagumya huku kila kampuni ikiwakilishwa na viongozi wao wakuu.
Mikataba hiyo imesainiwa kwa mujibu wa kanuni zilizoidhinishwa na Ewura na zinazosimamia uenderezaji wa miradi midogo ya kuzalisha umeme. Kampuni binafsi zinaruhusiwa kuendeleza miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati jadidifu(maji, upepo, jua tungamotaka) katika maeneo mahsusi kwa malengo ya kuuza umeme kwa wananchi au Tanesco.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Eng. Rubagumya alisema kuwa wawekezaji ambao wanategemea kuzalisha umeme na kuuza kwa Tanesco, mikataba maalumu ya kuuziana umeme inatakiwa kusainiwa baina ya wawekezaji husika na Tanesco.
Alisema kabla ya tukio la leo, Tanesco na Wawekezaji wa miradi sita ya kuzalisha umeme walikutana kwa lengo la kufanya maboresho kwenye mikataba ya kuuziana umeme. Mikataba iliyofanyiwa maboresho imepata idhini ya Ewura hivyo kupata baraka ya kusainiwa.
Aidha Tanesco imezipa kampuni hizo muda wa miezi 18 kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Kampuni sita zilizosaini mikataba ni; Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd inayomiliki mradi wa Ijangala Hydropower unaozalisha umeme wa maji kutoka maporomoko ya Mto Ijangala, wilayani Makate yenye uwezo wa kuzalisha 0.36MW.
Kampuni ya Madope Hydro Company Ltd, inayoendesha Mradi wa umeme wa Madope Hydropower 1.7MW, unaotokana na maporomoko ya maji ya Mto Madope wilayani Ludewa, Mkoa wa Njombe.
Kampuni ya Luponde Hydro Ltd, inayoendesha mradi wa Luponde Hydropower 0.9MW unaotoka na na maporomoko ya maji ya Mto Luhololo, wilayani Njombe.
Kampuni zingine ni; Kampuni ya Lung’ali Natural Resources inayoendesha mradi wa Maguta Hydropower 1.2MW umeme unaozalishwa kutoka maporomoko ya maji ya Mto Lukosi, wilayani Kilolo.
Kampuni ya Nextgen Solawazi Ltd inayoendesha mradi wa Kigoma Solar Power 5.0MW inayozalisha umeme wa jua eneo la Kigoma Special; Economic Zone.
Kampuni ya SSI Eenergy Tanzania Ltd ya Mradi wa Kahama Solar Power 10.0mw, umeme wa jua karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama. Miradi yote sita ina uwezo wa kuzalisha megawati 19.16.