Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (wakwanza kulia) akizungumza na Wanamuziki wa Injili (hawapo pichani) kuhusu azma ya serikali ya kuendeleza sekta ya sanaa hivyo na kuwataka watoe maoni ya mambo gani yaboreshwe kuendeleza tasnia hiyo, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa kwa wanamuziki wa injili alipokuwa akifungua Bunge.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (aliyeketi watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii wa Muziki Injili waliyohudhuria kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya sanaa kwa kundi la wanamuziki wa injili, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kikao hicho.
Msanii wa Muziki wa Injili Boniface Mwaitege akitoa ombi kwa serikali kuwasaidia wasanii wa Muziki wa Injili wanao dhulumiwa haki zao na moja ya kampuni (jina limehifadhiwa) ya usambazaji wa nyimbo za injili njia ya mtandao, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya sanaa kwa wanamuziki wa injili kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa wakati alipokuwa akifungua Bunge.
Msanii wa Muziki wa Injili Christina Shusho akitoa ombi kwa serikali la kuandaliwa kwa Tuzo za Muziki wa Injili nchini ili kutoa hamasa kwa wasanii hao, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya sanaa kwa wanamuziki wa injili kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa wakati alipokuwa akifungua Bunge.
Msanii wa Muziki wa Injili Emmanuel Mgaya akitoa ombi kwa serikali la kuangalia suala la gharama za kusajili Youtube Channel kuwa ni kubwa sana kwa kundi la wasanii, kwani wao hutumia akaunti hizo kutafuta masoko ya kazi zao na siyo kuhabarisha umma, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na Wanamuziki wa Injili kujadili mikakati ya kuendeleza tasnia sekta ya sanaa kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua Bunge.
Mtangazaji wa Kipindi Chomoza kinachotangaza Muziki wa Injili kutoka Televisheni ya Clouds James Temu akitoa ombi kwa serikali la wasanii kupata msaada wa kisheria ili kuwasaidia kupata haki zao kutokana na changamoto za mikataba mingi kuwa ya ulaghai, leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya sanaa kwa wanamuziki wa injili kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuendeleza Sanaa wakati alipokuwa akifungua Bunge.
………………………………………………….
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amezielekeza taasisi zinazosimamia Sekta ya Sanaa nchini kutoa ushauri wa kisheria bure kwa wasanii katika mikataba wanayoingia na wadau mbalimbali ili kuwasaidia kulinda maslahi yao.
Dkt.Abbasi ametoa agizo hilo leo Desemba 05, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na Wadau wa Muziki wa Injili ikiwa ni muendelezo wa vikao vyake vya kukutana na makundi mbalimbali ya Sanaa, kwa lengo la kujadili mambo bora ya kuendeleza tasnia hiyo kufuatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika hotuba yake alipokuwa akifunga Bunge.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Dkt.Hassan Abbasi aliwasihi wasanii hao wa Muziki wa Injili kukaa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kujadili kuhusu changamoto ya shirikisho lililopo kwa sasa ili waweze kuunda Shirikisho lililoimara ambalo litaweza kuwaunganisha wasanii hao na kuwasaidia kutatua changamoto zao.
“Serikali inatambua thamani ya Muziki wa Injili na haitaacha kuwasaidia na kuhusu kampuni hiyo inayowasumbua katika usambazaji wa kazi zenu kupitia njia ya kimtandao tumesikia kilio chenu na tunaenda kulifanyia kazi tutafuatilia usajili wao na namna wanavyoendesha biashara hiyo ili tuweze kuwachukulia hatua,” alisema Dkt.Abbasi.
Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali alisisitiza suala la maadili na Uzalendo k kwa wasanii ambapo alisema akiwa kama mlezi wa kundi hilo hatapenda kuona wasanii wakiwa mstari wa mbele kwa kukosa maadili.
Aidha, nae Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania Boniface Mwaitege aliomba Serikali kuwasaidia Wasanii wa Muziki wa Injili nchini kupata haki zao kutoka kwa moja ya Kampuni (jina limehifadhiwa) inayoingia mikataba na wasanii hao katika kusambaza kazi zao na badae kuwa dhulumu.
Halikadhalika naye Msanii wa Injili Christina Shusho alitoa ombi kwa Serikali kuandaa Tuzo za Muziki wa Injili ambazo zitasaidia kuleta hamasa ya ubunifu kwa wasanii hao katika kuandaa kazi bora zaidi.
Akihitimisha kikao hicho Dkt.Abbasi alisisitiza wasanii kuacha kukurupuka kusaini mikataba na wadau kabla ya kupata ushauri wa kisheria na pia alieleza kuwa serikali itakuwa ikitoa mialiko katika shughuli za kiserikali kwa kundi hilo kupitia shirikisho hivyo waunde umoja huo.