Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akisistiza jambo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo |
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwijuma alimaarufu “Mwana FA” kushoto akimueleza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ukubwa wa tatizo la maji wilayani Muheza wakati wa ziara yake |
MENEJA wa Ruwasa wilaya ya Muheza akieleza jambo wakati wa ziara hiyo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kulia akiteta
jambo na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu
Mwana FA na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na
kushoto ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
Mkurugenzi
wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara
yake wilayani Muheza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwijuma alimaarufu Mwana FA
*********************************
WIZARA ya Maji imehaidi kupelekea fedha wilayani Muheza Mkoani Tanga ili mradi wa kutoa maji eneo la Pongwe wilayani Tanga hadi Kitisa wilayani Muheza ulioishia njiani uweze kusambaa kwa wananchi ili kupunguza changamoto ya tatizo la maji wilayani humo.
Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo ambapo alisema fedha hizo ambazo makadirio yake ni Bilioni 4 watazipeleka kidogo kidogo mpaka zitakapokamilika
Alisema ni kweli fedha hizo ni nyingi lakini hawawezi kuzipata kwa mkupuo watakuwa wakipeleka kwa awamu wanaweza kutumia na kuangalia wapi wamebakiza na maelezo yake ni kwamba mradi mkubwa wa kutoa Maji Mto Pangani utakapoanza uungane na mradi ambao unaendelea.
“Niwahakikishie wananchi wa Muheza wizara ya maji haitakuwa kikwazo kuwapatia huduma ya maji najua tumechelewa hivyo mwezi Desemba tutawaletea fedha mfanye manunuzi ya mabomba na kabla ya mwezi huu haujaisha tuone mmeanza kuchimba mitaro na kulaza mabomba naliongea hili kwa sababu Rais Dkt John Magufuli alihakidi kwenye kampeni anataka wananchi wapate maji”Alisema
Aidha alieleza pia Rais Dkt John Magufuli alisema na serikali anayoiongoza haitavumilia kuona wananchi wanakosa maji na aliwalenga wananchi wanyonge hivyo raisi ametoa fedha kupitia mfuko wa maji na wanaangali maeneo yeye shida ya maji na wanapeleka na kueleza mradi wa maji wa Mto Pangani upo njiani.
“Lakini niwahaidi kwamba wizara ya maji haitakuwa kikwazo kwenye suala la maji wilaya muheza nimepitia ripoti kwa kweli hazipo vizuri kwenye wilaya ya Muheza na Mkinga kuna changamoto kubwa ya maji nimetoa maelekezo bahati nzuri wataalamu wa wizara ya maji wamekwisha kuingia wataanza kushughulika na Mkinga”Alisema
Alisema kwa bahati nzuri wilaya ya Muheza walikwisha kufanya kazi nzuri ya kutoa maji Pongwe mpaka Kitisa na yamesogea kilomita sita kuna bomba halijaakaa vizuri nalifahamu hilo ila kuna mradi mkubwa wa Mto Pangani lakini hatuwezi kusubiri mradi huo.
“Nafahamu kuna mradi mkubwa wa Mto Pangani lakini hatuwezi kusubiri mradi huo kama maji ya Tanga yanaweza kufika hapa na bahati nzuri Muheza tumeikabidhi Tanga Uwasa na nimekwisha kuwaeleza leo kwamba lazima huduma ya maji Muheza ifanane na Tanga mjini na Pangani kwa hiyo watashughulikia”Alisema
Awali akizungumza wakati wa ziara, Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma almaarufu Mwana FA alisema maji ndio tatizo kubwa kwenye Jimbo hilo na nililiahidi wakati wa kampeni na hata Rais alipotembelea mkoa wa Tanga tukiwa Korogwe nililihubiri suala hili.
Mbunge huyo alisema pamoja na kwamba serikali ya Rais Dkt John Magufuli inafanya kazi nyingi nzuri lakini hili la maji linawaweka kwenye wakati mgumu na watu hivyo wao wakamuomba tena mradi uliokuwa unatoa maji Pongwe Kilapura ambao ulikuwa na Tanki la lita laki saba ulikuwa umekwisha kuingiza maji NHC kwenye matanki.
Alisema lakini tatizo likawa kwenye mfumo wa usambazaji na kukawa na maeneo kwamba utafanayiwa kazi na hata Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alipokuja na kutoa namba zake akawa mdomo wazi kwamba kiasi cha fedha kinachoitajika ni bilioni 4 kwa hiyo mradi wa Bilioni 6.1 bado unahitaji bilioni 4 karibu asilimia 40 mradi haujakamilika.
“Ombi langu kwao toeni fedha kwenye mfuko wa maji japokuwa wazo la awali lilikuwa kusubiri mradi wa kutoa maji Mto Pangani utakaoanza mapema mwakani ingawa utachukua muda mpaka kukamilika na kufika kwa wananchi”Alisema Mbunge huyo.
Mbunge Hamisi alisema wanawashukuru wizara hiyo kwa kusikiliza ombi lake hivyo wanaomba huo mfumo wa utengenezwe kwa fedha kutoka mfuko wa maji halafu mradi wa kutoa maji Pangani utakapofika watoe kiasi kilichokuwa kimewekwa kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa usambazaji kiasi cha bilioni 4.
“Kama fedha zinarudi huko kwenye mradi mwengine zirudishwe huko lakini mfuko wa maji uwasaidie kwa sababu wananchi wanateseka niishukuru serikali ya awamu ya tano kuna sehemu maji yanatoka mara mbili kwa wiki na mara moja kwa wiki masaa manne”Alisema
Hata hivyo alisema pia kuna mahali maji yakitoka mara mbili kwa wiki unapigiwa simu tatizo hilo ni deni kubwa kwake na serikali ya awamu ya tano hivyo wanaomba lipatiwa ufumbuzi ili wananchi waweze kuondokana na adha hiyo.