Mhandisi uwekeza wa TANESCO Makao makuu Edetrude Zenda akimuelezea Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu utendaji kazi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo nchini Tanzania.
Baadhi ya wananchi mbalimbali wakipata maelezo kwenye banda la TANESCO wakati waliwapotembelea leo kwenye maonesho ya Bidhaa za viwandani yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kirwa jijini Dar es salaa,
Mhandisi Dismas Ngote akito mzelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika maonesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea kwenye viwanja wa Sabasaba barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
………………………………………..
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema umeme upo wa kutosha na uhakika ambao unaotosheleza matumizi ya viwanda vyote nchini.
Hayo yamesemwa na Mhandisi uwekeza wa TANESCO Makao makuu Edetrude Zenda
katika maonyesho ya viwanda yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam.
Maonesho hayo yamefunguliwa rasimi leo Desemba 03, 2020 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasimu Majaliwa.
Akifungua Maonesho hayo, Mhe. Majaliwa ametembelea banda la TANESCO na kulipongeza Shirika kwa kazi nzuri linayofanya.
“Mnafanya kazi nzuri kuhakikisha viwanda kote nchini vinapata umeme wakutosha na wa uhakika ili wasiwe na kisingizio cha kupandisha bei ya bidha zao” amesema Mhe. Majaliwa.
Mhandisi uwekeza wa TANESCO Makao makuu Edetrude Zenda alisema kiwango cha uzalishaji cha sasa ni MW 1601.84 ukilinganisha na matumizi ya juu ya nchi ambayo ni MW 1,177.2, hivyo kulifanya Shirika kuwa na uwezo mkubwa wa kuvipatia umeme viwanda.
Katika maonesho hayo TANESCO inatoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya huduma na utekelezwaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo mradi wa Julius Nyerere MW 2115.
Wateja waliofika katika banda la TANESCO walisema wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na TANESCO katika maonesho hayo na kuongeza wamepata fulsa ya kujifunza kuhusu mita za viwanda na jinsi zinavyofanya kazi.