Mawakala wakiwa katika zoezi la kuhesabu kura baada ya Uchaguzi huo. |
Bw. Danny Makange Msanifu Kilimo ambaye ni Katibu wa Baraza la michezo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumzia mipango mikakati ya baraza hilo jipya |
Picha ya Pamoja Ikionesha baadhi ya Viongozi wa Baraza la Michezo kutoka
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji baada ya kushinda katika uchaguzi
uliofanyika katika ofisi hizo Makao Makuu ya nchi Dodoma jana jioni,
kutoka kushoto ni Bi Fatma Mwera Afisa Kilimo wa Mkoa wa Dodoma ambaye
ni katibu msaidizi,katikati, Bw. Yassin Kazoba Mchumi, Mwenyekiti wa
Baraza la michezo na Bi Nyandaro Mapesi mtunza kumbukumbu ambaye ni
Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo.
Na MwandishiWetu Dodoma
Viongozi
wa Baraza la Michezo wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliochaguliwa katika kinyanganyiro
kikali cha kugombea nafasi za Mwenyekiti na Mwenyekiti Msaidizi wa Michezo,
pamoja na nafasi ya Katibu mkuu na Katibu mkuu msaidizi, wameapa kukuza tasnia ya
michezo katika Taasisi hiyo nakutumia fursa walioipata kutangaza shughuli za Tume
ya Taifa ya Umwagiliaji kupitia sekta ya Michezo.
Akizungumza
baada ya uchaguzi huyo Mwenyekiti aliyeshinda Bw. Yassin Kazoba Ambaye ni mchumi,
ametoa ahadi yakushirikisha watumishi wote wa Tume katika shughuli za michezo kwani
Utendaji wa kazi unategemea afya za watumishi.
Katibu
wa Baraza hilo jipya Bw. Danny Makange alisema anamkakati wakuainisha wachezaji
katik a Ofisi za Tume nchi nzima ilikuweza kupata ushindani katika michezo ya mabonanza
na mashindano mengine na mashirika naTaasisi za Serikali.
Pia
kuunganisha wanamichezo na wadau ilikuwezesha taasisi na shughuli zake zifahamike.
Kwa upande
wake Mkurugenziwa Utawala na Rasilimali watu Bi, MARY MWANGISA amewataka viongozi
hao pamoja na kutekeleza wajibu katika shughuli za michezo, waongeze bidii ya kazi
ili Taasisi hiyo iweze kufikia malengo ya kimkakati la kukuza eneo la
Umwagiliaji zaidi la Hekta zaidi laki sita zinazomwagiliwa kwasasa,kufikia Hekta
Milioni moja na laki mbili ifikapo mwaka 2025.
Awali
Mwenyekiti wa uchaguzi huoBw, Godwin
Mutahangarwa ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha sheria, amewataka viongozi hao
kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kuushukuru uongozi wa Taasisi kwa kuunda chombo
hicho ambacho ni muhimu sana na namna mojawapo yakuwashirikisha wafanyazaki na kujenga
uhusiono mwema kati ya wafanyakazi na Taasisi naTaasisi.