Wiki moja baada ya kampuni ya simu za mkononi ya TECNO kutangaza kutoa zawadi ya kitita cha Shilingi milioni moja pamoja na zawadi ya kuwapeleka Hifadhi ya Ngorongoro washindi wa kampeni ya CAMON 16 BILLBOARD STAR, tayari imefanikiwa kuwapeleka baadhi ya wateja wake na wafuasi wake wa kurasa za mtandaoni walioshiriki na kuchaguliwa kama washindi wa ziara hiyo.
Picha ya Pamoja ya washiriki wa CAMON 16 TOUR
Akizungumza jijini Dar es Salaam, meneja masoko mtandaoni Bi. Salma Shafi amesema ziara hiyo ilikuwa ni kutimiza ahadi waliyoitoa kwenye kampeni yao ya CAMON 16 BILLBOARD STAR na kwamba ziara hiyo ililenga kufanya uzoefu wa kupiga picha kwa kutumia simu ya TECNO CAMON 16.
“Tunatimiza ahadi yetu kwa watu wetu katika kile tulichoahidi kwenye kampeni ya CAMON 16 BILLBOARD STAR na sasa tumehitimisha na TECNO CAMON 16 TOUR ambayo tumetembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ili wale wote walioshiriki katika ziara hii waweze kupata uzoefu wa picha zinazopigwa kwa kutumia TECNO CAMON 16” amesema Bi. Salma.
Washiriki wa CAMON 16 TOUR wakiongozwa na Elizabeth Michael wakipiga selfi kwa Camon 16
Bi. Salma ameongeza kuwa ziara hiyo katika Hifadhi ya Ngorongoro ililenga kuwapa fursa washiriki katika kupiga picha zenye kuvutia na mazingira ya asili kwa kutumia kamera bora ya simu ya TECNO CAMON 16 ambayo imeingia sokoni hivi karibuni.
Ziara hiyo pia iliambatana na balozi wa TECNO CAMON 16 Elizabeth Michael maarufu kama LULU ambaye pia ni mwigizaji wa Bongo movie pamoja na mpiga picha maarufu Bwana Danniel Msirikale .
Elizabeth Michael (Lulu) akitumia Camon 16 kupiga selfie (Picha imechukuliwa na Camon 16)
Kwa upande wao washiriki wameelezea hisia zao za ziara hiyo ya Camon 16 kuwa ilikuwa ni fursa ya kipekee kwao kutembelea maeneo mbalimbali ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na kuchukua uzoefu wa kupiga picha kwa kutumia kamera ya simu ya TECNO CAMON 16.
Bwana Mohamed Hussein ni miongoni mwa washiriki, amesema yeye binafsi hajawahi kufika katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, hivyo anaishukuru kampuni ya TECNO kwa kutoa fursa hiyo kwa watu wake.
“Kiukweli sikawahi kuja Ngorongoro, hii ni mara yangu ya kwanza, kwakweli nawashukuru sana TECNO kwa kutujali lakini kilichonishangaza zaidi ni simu hii ya Camon 16 ina picha kali sana kwakweli kwa mtu anayependa picha hii simu ataifurahia sana” amesema Bwana Mohamed.
Washiriki wa CAMON 16 Tour wakiendelea kupata uzoefu wa kupiga picha kwa kamera ya TECNO CAMON 16.
Ikumbukwe kuwa TECNO CAMON 16 ni simu toleo jipya kabisa na tayari imeingia sokoni ikiwa na sifa nzuri hasa upande wa kamera yenye MP48 na flashi nne, Memori kubwa GB 128 pamoja na skrini kubwa ya inchi 6.6. Taarifa zaidi tembelea ukurasa wa TECNO instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/