*****************************************
Serikali imesema katika kipindi cha pili cha awamu ya pili ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itajikita zaidi katika kuboresha uwekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kujenga uchumi wa nchi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini na kuongeza kuwa baada ya kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli kujikita katika uwekezaji mkubwa wa maeneo ya miundombinu na nishati pamoja na huduma za kijamii sasa serikali inalenga kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi……Insert Prof Palamagamba John Kabudi
Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Mhe. Frederic Clavier amemkabidhi Prof Kabudi barua ya iliyoandikwa na Rais wa Ufaransa Mhe Emmanuel Macron kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kumpongeza kwa kuiwezesha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ikiwa ni miaka mitano kabla ya muda uliopangwa ….Insert Balozi wa Ufaransa
Pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa Nchini Mhe Manfred Fanti ambapo Balozi Fanti ameweleza Waziri Kabudi kuwa pamoja na kamati ya mambo ya Nje ya Bunge la Umoja wa Ulaya kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu Tanzania bado umoja hakuna maazimio yeyote yaliyofikiwa kuhusu Tanzania na kwamba Umoja wa Ulaya utaendelea kuimarisha mahusiano mazuri na ya kihistoria yaliopo kati ya Tanzania na Umoja huo.
Balozi Fanti ameihakikishia Tanzania kuwa Umoja Ulaya utatekeleza miradi yote iliyopangwa kutekelezwa Nchini kwa ufadhili wa Umoja huo.
Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (International Residual Mechanism for Criminal Tribunals -IRMCT)na Bwana Abubacar Tambadou.
Katika mazungumzo yao Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (International Residual Mechanism for Criminal Tribunals -IRMCT)na Bwana Abubacar Tambadou amemweleza Waziri Kabudi kuwa amefika kujitambulisha baada ya kupata uteuzi huo lakini pia kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano unaoutoa kwa Mahakama hiyo na kuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kuiwezesha kutimiza majukumu yake.