TAARIFA YA KIFO.
TAREHE 26.11.2020 MAJIRA YA 19:00HRS HUKO KATIKA KATA YA MANTARE, WILAYA YA KWIMBA, MKOA WA MWANZA, ILIPATIKANA TAARIFA YA MTOTO PENDO PHILIPO, MIAKA 8, MSUKUMA, MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA, S/M ISHINGISHA, MKAZI WA ISHINGISHA, KUWA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA FISI SEHEMU ZA MWILI WAKE. INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NA WATOTO WENZAKE 3 WAKIOKOTA KUNI PORINI NDIPO FISI ALIWAFUKUZA NA KUMJERUHI MAREHEMU HADI KUSABABISHA KIFO CHAKE. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA NA VYOMBO VINGINE VYA DOLA KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA YA WANYAMAPORI LINAFANYA JITIHADA ZA KUMDHIBITI FISI HUYO ILI ASILETE MADHARA KWA WANANCHI NA WATOTO WENGINE. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUTOA WITO, KUWAONYA WAZAZI NA WALEZI KUACHA TABIA NA MAZOEA YA KUWATUMA WATOTO WADOGO PEKE YAO PORINI, KWANI WANAWEZA KUKUTANA NA WANYAMA WAKALI PIA WANAWEZA KUFANYIWA VITENDO VYA KIKATILI NA BINADAMU WABAYA