Home Siasa CCM ILEMELA WAMPONGEZA RAIS JPM, MBUNGE NA MADIWANI KWA USHINDI

CCM ILEMELA WAMPONGEZA RAIS JPM, MBUNGE NA MADIWANI KWA USHINDI

0

****************************************


Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela kwa pamoja wametoa tamko la kumpongeza aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho Rais Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mgombea ubunge Mhe Dkt Angeline Mabula, madiwani wote  19 wa kata za jimbo hilo na wale wateule kupitia viti maalum kwa ushindi mkubwa na wa kishindo.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa kikao maalum cha halmashauri kuu ya wilaya hiyo kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Nelson Mesha kikiwa na lengo la kutathimini namna zoezi zima la uchaguzi lilivyoendeshwa ndani ya wilaya hiyo ambapo kwa pamoja wakakubaliana kuridhishwa na jitihada na mchango wa kila mwanachama katika kukipatia ushindi chama hicho sanjari na kukubaliana kuwapongeza wagombea wote wa chama chao kwa ushindi wa nafasi mbalimbali za uchaguzi uliofanyika nchini mwezi Oktoba 25, ambapo katika wilaya hiyo mgombea wa nafasi ya Urais alipata ushindi kwa asilimia 91 na mbunge akishinda kwa asilimia 84 huku kata zote 19 zikichukuliwa na wagombea wa chama cha mapinduzi

‘.. Wakati wenzetu wakiendelea kulalamika duniani sisi tunajipanga kuchapa kazi, CCM wilaya ya Ilemela leo tunatoa tamko rasmi la kumpongeza Rais Dkt John Magufuli, Mbunge Dkt Angeline Mabula na madiwani wa kata zote kwa ushindi wakiwemo na wale wa viti maalum ..’ Alisema mwenyekiti huyo

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula akawatakia kheri ya utekelezaji mwema wa Ilani ya uchaguzi wagombea hao walioshinda nafasi mbalimbali za uchaguzi  huku akisisitiza kuwa ushindi huo unaashiria kuwa na Ilemela ya Kijani

Akihitimisha mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuwashukuru wanachama wa chama cha mapinduzi na wananchi kwa ujumla kwa kukiamini chama chake na kuwapigia kura za ushindi wagombea wote wa chama hicho akaahidi kufanya ziara kwa wanachama na wananchi katika maeneo yao wanayoishi ili kusikiliza ushauri, kero na changamoto zinazowakabili na kisha kuzipatia ufumbuzi sambamba na kuipongeza kata ya Kahama kwa kitendo cha wananchi wake kuongoza katika kujitokeza kupiga kura kwa zaidi ya asilimia 99.3, Kata ya Mecco kwa kuwa ya pili kwa asilimia 91 na ya tatu ikiwa Kayenze kwa