MKURUGENZI
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt James
Mataragio akizungumza na wachezaji wa timu za shirika hilo ambazo
zinashiriki kwenye michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye
viwanja mbalimbali mjini hapa.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt James
Mataragio kulia akiwa na Katibu wa Michezo wa Shirika hilo Elinaike
Naburi wakiwasikiliza watumishi wa shirika hilo ambao ni wanamichezo
wanaoshiriki mashindano ya Shimuta Jijini Tanga
Mmoja
wa wachezaji wa timu ya TPDC akichangia jambo wakati wa kikao hicho na
Mkurugenzi wa TPDC Dkt James Mataragio ambaye hayupo pichani
Mmoja wa wachezaji wa timu ya TPDC akichangia jambo wakati wa kikao
hicho na Mkurugenzi wa TPDC Dkt James Mataragio ambaye hayupo pichani
Sehemu
ya watumishi wa TPDC ambao wanashiriki mashindano ya Shimuta Jijini
Tanga wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika hilo Dkt James Mataragio
Sehemu ya watumishi wa TPDC ambao wanashiriki mashindano ya Shimuta
Jijini Tanga wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika hilo Dkt James
Mataragio
Mkurugenzi
wa Shirika hilo Dkt James
Mataragio wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ua pamoja na
wachezaji wa timu za shirika hilo ambazo zinashiriki mashindano ya
Shimuta
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Dkt James Mataragio amesema wameyatumia mashindano ya Shimuta yanayoendelea Jijini Tanga kama njia ya kujitangaza hivyo yatakuwa na tija kwao kutokana na kwamba wamekuwa wakifanya biashara ya kuuza gesi na shughuli za kutafuta mafuta.
Dkt Mataragio aliyasema hayo leo jijini Tanga wakati akizungumza na wachezaji wa timu za shirika hilo ambazo zinashiriki kwenye michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali mjini hapa.
Mkurugenzi huyo ambaye alifika Jijini Tanga leo asubuhi kushiriki katika timu yao inayoshiriki kwenye mashindano ya Shimuta amesema wamekuwa washiriki wazuri kwa miaka mingi.
Alisema kila siku Shirika hilo limekuwa na timu ya ushindi ambapo wamekuwa wakifanya hivyo katika mashindano mbalimbali huku akieleza mwaka huu wamekuwa mahiri kwa kuweza kuleta ushindani.
Aidha alisema umahiri huo umesaidia kuleta ushindani kwenye michezo mbalimbali kwa mfano mchezo wa Wavu,Kikapu,Riadhaa,Karata ,Pete na Mpira wa Miguu ambapo wameshiriki kote na kuweza kushinda vikombe sita na kupata medali moja lakini kikubwa zaidi wamejenga afya ya wafanyakazi wao.
“Ushiriki wetu umekuwa na umuhimu kwa sababu michezo ni afya na inaongeza tija kwa hiyo mimi kama Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC nalitambua hilo na ndio maana siku zote nawatia moyo vijana wetu kushiriki kwenye michezo kwa sababu najua michezo inaleta tija”Alisema
“Lakini kikubwa zaidi sisi kama TPDC ni shirika la Serikali ambalo linafanya biashara ya kuuza gesi na shughuli za kutafuta mafuta hivyo kushiriki kwenye michezo hiyo ni kuitangaza TPDC na shughuli ambazo tunazifanya “Alisema