MABAO ya Josip Ilicic dakika ya 60 na Robin Gosens dakika ya 64 yameipa Atalanta ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Liverpool usiku wa jana kwenye mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Anfield. Pamoja na kupoteza mchezo huo, Liverpool inaendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi zake tisa, mbili zaidi ya Ajax inayofuatia ikiizidi wastani wa mabao tu Atalanta, wakati Midtjylland inashika mkia haina pointi baada ya timu zote kucheza mechi nne PICHA ZAIDI SOMA HAPA