Home Mchanganyiko MBUNGE AAHIDI MSIKITI ULIOHARIBIWA NA UPEPO KUREKEBISHWA NDANI YA WIKI MOJA

MBUNGE AAHIDI MSIKITI ULIOHARIBIWA NA UPEPO KUREKEBISHWA NDANI YA WIKI MOJA

0

Muonekano wa msikiti  wa Nyakanazi baada ya kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha novemba 21, mwaka huu na kusababisha changamoto katika utekelezaji wa ibaada kwa waislamu.

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi  Mhe. Mhandisi Ezra John Chiwelesa mwenye shati la drafti  akikagua uharibufu wa msikiti pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo diwani wa kata ya Rusahunga Mhe. Amosi Josephat aliyebeba koti.

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi  Mhe. Mhandisi Ezra John Chiwelesa kulia akiteta jambo na imaamu mstaafu wa msikiti Nyakanazi Ust. Mbaraka Mrisho mara baada ya kujionea namna msikiti ulivyoharibika.

……………………………………………………………………………………….

Na Allawi Kaboyo – Biharamulo.

Mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha novemba 21, mwaka huu ilisababisha madhara makubwa ikiwemo kuezuliwa kwa msikiti mkubwa uliopo mji mdogo wa Nyakanazi kata Ya Rusahunga wilayani Biharamulo na kusababisha adha kubwa kwa waumini wa dini ya kiislamu katika utekelezaji wa ibaada.

Taarifa iliyotolewa na imaamu mstaafu wa msikii huo Ustadhi Mbaraka Mrisho mbele ya mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi alipofika msikini  hapo novemba 25, mwaka huu, imeeleza kuwa  mvua hiyo ilinyesha majira ya saa saba mchana na kusababisha madhara hayo hali inayopelekea sasa ufanyaji wa ibaada kusuasua kutokana na hali ya hewa ilivyo kwasasa.

Mrisho amesema kuwa licha ya kutokea kwa maafa hayo hakukutokea madhara yoyote kwa Binadamu hivyo watu wote wapo salama licha ya kuwa changamoto iliyopo sasa ni namna ya ufanyaji  wa ibaada, ambapo ametumia fursa hiyo pia kuwaomba wadau kuweza kuchangia ili msikiti huo urudi katika hali yake ya kawaida.

Amesema kuwa baada ya tathimini kufanyika gharama za kurekebisha msikiti huo hadi kukamilika kwake ni zaidi ya shilingi milioni 6.5.

Kwaupande wake mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi Mhandisi Ezra John Chiwelesa amewapa pole waumini wa dini ya kiislamu wanaotumia msikiti huo baada ya kujionea hali halisi ilivyo na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki huku utaratibu wa kuirejesha nyumba hiyo ya ibaada kwenye hali yake ya kawaida ukiwa unaendelea.

Chiwelesa amesema kuwa nyumba za ibaada zinapaswa kupewa kipaumbele kwa kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakizitumika mara nyingi kuwaombea viongozi pamoja na taifa kwaujumla hasa kwenye kipindi cha janga la CORONA na hata kipindi cha uchaguzi mkuu.

“Nyumba hizi za ibaada ni muhimu sana kuzijali na kuzingalia maana zimekuwa zikitumika kutuombea sisi viongozi lakini na watanzania kwa ujumla, niseme tu nimefika na nimejionea mwenyewe niwatoe wasiwasi ndugu zangu waislamu msikiti huu utajengwa na utaanza kutumika kwa muda mfupi.” Amesema Mhandisi Ezra

Amesema kuwa yeye kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo mungu akipenda atahakikisha msikiti huo unarekebishwa na kurudi katika hadhi yake ndani ya wiki moja,, ambapo ametoa wito kwa wadau mbalimbali  kumuunga mkono ili kuhakikisha nyumba hiyo ya ibaada inasimama upya na waumini wanaendelea na ibaada kama kawaida.