Na John Walter-Manyara
Mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti amewakaribisha wawekezaji kufika katika mkoa huo na kuwekeza kwenye Saruji kwa kuwa mkoa huo katika wilaya ya Hanang’ una madini ya kuzalisha bidhaa hiyo .
Mkuu huyo wa mkoa akizungumza na kituo hiki amesema ni wakati wa Wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kufika mkoani hapo na kujenga Kiwanda cha Saruji ili kusaidia upungufu wa Malighafi hiyo.
“Katika maeneo ya Hanang’ kumegundulika kuwepo kwa malighafi ambayo inaweza kuzalisha Simenti, kwa hivyo serikali ya mkoa tunachukua frusa hii kuutangazia Umma kwamba wawekezaji wafike kuitumia Fursa hii” alisema Mkirikiti
Hivi karibuni mikoa mbalimbali ukiwemo wa Manyara imeshuhudiwa bei ya Saruji ikipanda ghafla baada ya ya viwanda vinavyofanya uzalishaji kukosa Malighafi.
Mkirikiti amesema baada ya kujua hilo waliangalia uhalisia na kugundua kuwa Saruji imeanza kuja na sasa wanachunguza nani anaepandisha bei na endapo atabainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mkirikiti amewaondoa hofu wananchi wa mkoa huo na kuwaeleza kuwa Simenti ipo na inapatikana kwa bei inayotambulika na serikali.
Saruji katika mikoa mingi hupatikana kwa shilingi 15,000 lakini kwa sasa baadhi ya Mawakala wanauza hadi shilingi 19,000 wakidai kuwa inatokanana na gharaza za ziada wanazotozwa kwenye usafiri kwa kuwa wanatumia muda mrefu kusubiri Saruji hiyo.