Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr.  Tulia Ackson anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Fainali za shindano la urembo  la Miss Tanzania litakalofanyika tarehe 5 Desemba 2020 katika ukumbi wa  Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Yenye kauli mbiu ya ‘urembo ni heshima’ 

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look Bi. Basilla Mwanukuzi ambao ndio waandaaji  na waratibu wa shindano hilo kubwa lenye hadhi hapa nchini amejulisha Vyombo  vya Habari kwamba Mheshimiwa Tulia Ackson amethibitisha kuwa Mgeni Rasmi wa  shindano hilo.  

Hii ni mara ya tatu mfululizo Kampuni ya The Look inaandaa shindano hilo tangu  mwaka 2018 walipochukua umiliki kutoka kwa waandaali wa mwanzo. Naibu Spika Mheshimiwa Tulia Ackson ni mwanamichezo, mpenda sanaa na kinara  katika shughuli zinazoweka kipaumbele katika kusaidia jamii na amekuwa  akifuatilia kwa karibu mashindano haya ambayo yanaendeshwa kwa malengo ya  mashindano ya dunia ya ‘beauty with a purpose’ na yamekuwa yakitoa fursa  mbalimbali kwa wasichana na wadau wengine wa tasnia ya urembo.  Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, ambapo wasichana 20 kutoka mikoa  mbali mbali ya Tanzania wamefuzukuingia fainali. 

Licha ya changamoto ya ugonjwa wa korona mwanzoni mwa mwaka kumekua na  wito mkubwa sana wa warembo wenye vigezo vya kushiriki mashindano kujitokeza  samabamba na vigezo mwaka huu warembo wote 20 wana miradi yao ya kusaidia  jamii BWAP ‘Beauty with a purpose project’ ambazo nazo zitashindanishwa na  project moja itaibuka kidedea.

Shindano la mwaka huu linatarajiwa kua na msisimko wa aina yake kutokana na  maandalizi mazuri na warembo waliofuzu fainali kua na vigezo vya hali ya juu vya  mashindano ya dunia. Warembo waliofuzu kuingia fainali ni kama ifuatavyo;- 

  1. PRISCA LYIMO – UBUNGO DSM 
  2. TAMIA HAKAM – ARUSHA  
  3. JULIANA RUGUMISA – ARUSHA  
  4. REHEMA CUTHBERT – ARUSHA  
  5. YVONNE PAUL – KIGAMBONI 
  6. RUTH BENITHO – ILALA 
  7. GRACE MACHIBULA – UBUNGO 
  8. ROSE MANFERE – TEMEKE DSM  
  9. MARGARET MWAMBI – KIGAMBONI DSM  
  10. SARAFINA MAGEYE – KINONDONI 
  11. MARTHA GOLODI – UBUNGO DSM  
  12. ZENITHA CHUNDU – MOROGORO  
  13. DEOLYN MOLLEL – MOROGORO  
  14. HOYCE BAKANOBA – TABORA  
  15. NECERIAN KIVUYO – DODOMA  
  16. RAZIA ABRAHAM – KINONDONI DSM  
  17. ANGELA PENDAELI – ARUSHA 
  18. ADVERA MWEMBA – MWANZA  
  19. VERYNICE DEOKARI – KINONDONI DSM  
  20. GLORIA FELA – ILALA DSM