……………………………………………………………………………
Shirikisho la Soka Dunia FIFA limemfungia miaka mitano Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad,kutojihusisha na masuala ya soka kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi yake ikiwa ni matumizi mabaya ya fedha pamoja na kujipatia zawadi binafsi kwa jina na shirikisho la soka Africa (CAF).
Maamuzi ya kamati hiyo yanakuja ikiwa Rais Ahmad ambaye anatoka nchi ya Madagascar tayari alikuwa ametangaza kuwania muhula wa pili wa CAF uchaguzi unaotarajia kufanyika mwezi Machi mwakani.
Hivyo kuchaguliwa kwa awamu ya pili kunategemea endapo atashinda kesi ya rufaa aliyoiwasilisha katika Mahakama ya kutatua mizozo ya CAS, huku kesi hiyo akihakikisha inasikilizwa mapema ili kumruhusu kuthibitishwa kuwa mgombea.