…………………………………………………………….
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo amezindua kisima cha Maji katika Mtaa wa Mayeto-Hombolo Makulu ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kutatua kero ya maji kwa wananchi.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mavunde amesema kisima hicho ni utekelezaji wa ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi kutatua kero hiyo.
Amesema kisima hicho kitawanufaisha zaidi ya wananchi 2000.
“Kisima kimekuwa faraja kubwa kwa wananchi wa Mayeto ambao walikuwa wanatembea kufuata maji kwa zaidi ya kilomita tano,”amesema.