vlcsnap-2020-11-22-17h23m52s009.png

NA RAHEL NYABALI

……………………………………………………………………..

KIGOMA.

Wajasiliamali na wafanya biashara wadogo wadogo Wanawake Mkoani Kgoma wameziomba taasisi za kifedha ambazo zinatoa mikopo kupunguza masharti ya utoaji na ulipaji wa mikopo hiyo ili  hatua ambayo itaweza kuwasaidia kukuza mitaji yao.

Yameelezwa hayo katika  semina iliyo andaliwa na Benki ya CRDB iliyo lenga kuwainua  wanawake wajasiriamali, kiuchumi kuondokana na mikopo umiza waliyo kuwa wanachukua mitaani.

Eppifania kagoye  na Sesilia Funga nibaadhi ya wajasilia mali mkoani humo wamesema kuwa  taasisi nyingi za kifedha ambazo zinapitikana mitaani  zimekuwa zikitoa riba kubwa hivyo kusababisha biashara za wanawake wengi  kuzidi kudumaa .

Akisisitiza wanawake kufungua akaunti ya Malkia  ambayo inatoa fursa kwa wanawake kujipatia mikopo, Rachel senni ambaye ni  meneja wa huduma kwa wanawake amesema huduma hiyio itasaidia kuinua kundi kubwa la wanawake ambao  walishindwa kufikia Marengo yao.

Saidi pamui ni meneja CRDB kanda ya Magharibi amesema lengo la benki hiyo ni kuunga juhudi za serikali  kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu ikiwa na lengo la kukuza  mitaji ya wajasiriamali na wafanya biashara.