Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti Sao Hilll Juma Mwita Mseti aliwaasa watumishi kuelewa mada zote zitakazotolewa ili kuhakikisha kunakuwa na uelewa wa pamoja katika kuhakikisha malengo yanayoweka kufikiwa kwa wakati na hatimaye kufikia malengo ya taasisi nzima
Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Sao Hill wakiwa kwenye mafunzo ya kuboresha utendaji wa kazi
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
Watumishi
wa Shamba la Miti Sao Hill wanapewa mafunzo ya mfumo wa wazi wa mapitio ya
utendaji kazi ambayo yanalenga kuwakumbusha watumishi juu ya ujazaji wa fomu
hizo ili kufikia malengo ya taasisi.
Mafunzo
haya yanawakumbusha watumishi pia juu ya upangaji wa wa malengo
,utekelezaji, ufuatiliaji na mapitio ya utendaji kazi ili kufikia malengo
waliyojiwekea.
Akiwapa
mafunzo hayo Mkufunzi wa mafunzo hayo Frank Kamugisha aliwataka watumishi
kutumia mafunzo haya kama sehemu ya kujikumbusha na hivyo kuhakikisha mafunzo
haya yanaendelea kuwasaidia katika kufikia malengo ya taasisi.
Naye
Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti Sao Hilll Juma Mwita Mseti aliwaasa watumishi
kuelewa mada zote zitakazotolewa ili kuhakikisha kunakuwa na uelewa wa pamoja
katika kuhakikisha malengo yanayoweka kufikiwa kwa wakati na hatimaye kufikia
malengo ya taasisi nzima.
Kwa
upande wake Afisa utumishi wa shamba
hilo Felista Bayo alisema kuwa mafunzo haya ni muhimu kwani yanatasadia katika
utendaji wa kazi wa kila siku na hivyo kufanya kila mtumishi kuwajibika katik
nafasi yake kulingana na malengo yaliyowekwa.
Lakini
pia afisa habari Mwanaisha Luhaga alisema
kuwa Mafunzo hayo yanawasaidia kuwakumbusha wajibu wao katika kazi wanazozifanya
za kila siku kwani bila kuwa na malengo hawawezi kuwa na utekelezaji wenye
tija.
“Hapa
tunafundishwa jinsi ya kuweka malengo, utekelezaji ,ufuatiliaji na mapitio ya
utendaji kazi.Hii inasaidia sana kufikia malengo ya taasisi kwani tuna uhakika
kila mmoja atatimiza wajibu wake na kwa wakati” Luhanga
Mafunzo
hayo yanatolewa na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
kwa kushirikiana TFS ambayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 16
Novemba 2020.