***********************************
Mcheza Golf George Sembi wa TPC Amefanikiwa kubakiza ubingwa Nyumbani baada ya kuibuka kinara katika Mashindano ya Wazi ya TPC yaliyomalizika Jana (Jumapili) Moshi Mkoani Kiimanjaro.

Mchezaji huyo alibuka na Ushindi Baada ya kupiga Mikwaju 147 akifuatiwa na Vicent Gulo wa TPC aliyefungana na Isihaka Daudi wa Lugalo ambaye ameshika nafasi ya Tatu kwa Mikwaju 149.

Kwa Upande wa Divisheni A Mshindi ni Nahuum Gabriel aliyepata Mikwaju ya Jumla 147 akifuatiwa na Juma Mcharo aliyepiga Mikwaju ya Jumla 148.

Kwa Upande wa Divisheni B Mshindi ni Private Laurent Sangawe aliyepiga Mikwaju ya Jumla 149 akifuatiwa na Private Haridi Shemdolwa wote wa Lugalo Baada ya kupata Mikwaju ya jumla 152.

Divisheni C Mshindi ni Sahif  Kanabhai wa Arusha baada kupiga Mikwaju ya Jumla 154 akifuatiwa na Issa Issa wa TPC kwa Mikwaju ya Jumla 147.

Kwa Upande wa Wanawake Mshindi ni Madina Iddi kwa Mikwaju ya jumla  146 akifuatiwa na Neema Ulomi wote hao ni wa Arusha huku kwa wazee Ashik Nanabhai wa Arusha akiibuka mshindi.

Kwa upande wa Watoto Viwanja Tisa Mshindi ni Zacharia George na Viwanja 18 Mshindi ni Ibrahim Gabriel kwa Mikwaju ya Jumla 145.

Akizungumza katika Sherehe za Ufungaji wa Mashindano hayo Nahodha wa Klabu ya TPC Jaffary Ally amevishukuru vilabu vilivyoleta Wachezaji na Kuwapongeza wachezaji wakulipwa kwa utaalam walionyesha katika Mashindano hayo.
Kwa Upande Meneja kitengo cha huduma za kifedha kwa sekta ya kilimo biashara kutoka Benki ya CRDB waliodhamini mashindano hayo alisema Benki  iko tayari kusaidia michezo bila kubagua.