Katika kuendeleza mkakati wake wa kuimarisha usalama mahali pa kazi, kampuni ya TBL Plc iliandaa mafunzo ya kuzima moto kwa wafanyakazi wake katika kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam, ambayo yalitolewa na wataalamu kutoka jeshi la zima moto na uokoaji nchini.
Mtaalamu kutoka Jeshi la zima moto na uokoaji nchini, Sajenti Katonga Omary, akitoa mafunzo ya kuzima moto kwa wafanyakazi wa TBL Plc.
Meneja Mawasiliano wa TBL Plc,Amanda Walter, akifanya majaribio ya kuzima moto wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Plc waliohudhuria mafunzo ya zimamoto katika picha ya pamoja na wakufunzi wao kutoka Jeshi la zima moto na uokoaji