
Chama Tadea kimesema ni vyema mashirika ya haki za binadamu yakatoa taarifa za kuwaonya wanasiasa wanapotoa matamshi ya kuhatarisha amani na kutozishutumu serikali zikizo madarakani.
Pia kimesisitiza si haki na si wajibu kwa mashirika hayo kuonekana yakijiegemeza kwenye lawama na kuacha kutoa ushauri mapema.
Makamo Mwenyekiti wa ADA Tadea Juma Ali Khatib ameeleza hayo kufuatia taarifa iliotolewa na kamisheni ya haki za binadamu zilizodai kuna watu 150 wamekamatwa na polisi.
Khatib amesema zipo kauli za baadhi ya viongozi wa upinzani ambazo ziliekekeza moja kwa moja kutaka yatokee machafuko,fujo na uvunjifu wa amani.
Amesema pamoja na mashirika ya haki za binadamu kuwepo yamefumba macho na kutosikika yakilaani au kuonya
Amesema mtindo wa kujiegemeza katika muktadha wa kulaumu kuliko kuasa na kuonya mapema hakuonyeshi haki na usawa.
Khatib amesema kutoushutumu upinzani nako hakuutoshi kukuza ufanusi badala yake yasimame kati kati ili kuonyesha utendaji wenye mizania.
Hata hivyo Katibu mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba ya SMT , Profesa Sifuni Mchome amesema Serikali haijapata taarifa hiyo na huenda hao wamekamatwa kisheria
Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa na Kamishina wa Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Michelle Bachelet limedai viongozi wa upinzani na wafuasi wao wamekamatwa Oktoba 27.
Michelle amesema watu haovwametiwa mbaroni siku moja kabla ya kupiga kura na kuelezea wanavyosikitishwa.
Serikali kupitia Profesa Mchome imesema bado haijapata taarifa hiyo na kama ni madai ya watu kukamatwa ni kwa mujibu wa sheria si vinginevyo.


