
**********************************
Na Allawi Kaboyo.
Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi ameapa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo ikiwa ni moja ya ndoto zake za kuleta maendeleo ambayo wananchi waliomuamini wamekuwa wakiyatamani kuyaona kwa kipindi kirefu.
Akiongea nje ya Jengo la Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mara baada ya kula kiapo hicho Mhe. Mhandisi Ezra John Chiwelesa ammesema kuwa ubunge huu alioupata sio wake bali ni imaani kubwa aliyopewa na wananchi wa Biharamulo hivyo anawajibika kuwatumikia kwa kutekeleza ahadi alizozitoa pamoja nakuitekeleza Ilani ya chama chake.
Mhhe. Ezra amesema kuwa Halmashauri ya Biharamulo haina sababu ya kuwa miongoni mwa halmashauri za mwisho kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhesabiwa kwenye halmashauri ambazo wananchi wake ni Masikini wakati vipo vyanzo vingi vya mapato kwenye wilaya hiyo.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano kipindi cha pili watajitahidi kuwa na baraza bora la madiwa ambalo itasimama kwaajili ya kuwatetea wananchi pamoja na kusimamia mapato ii kuweza kukuza uchumi wa wanabiharamulo ambapo ameongeza kuwa atatuia muda mwingi jimboni kufanya kazi za wananchi pale atapokuwa hana vikao vya bunge.
Akizungumzia ahadi yake ya kumuajili mwanasheria kwaajili ya kutoa msaada wa kisheria, Ezra amesema kuwa ahadi hiyo ipo pale pale na atahakikisha wananchi wenye matatizo ya kisheria wanapatta mmsaada huo bure bila kulipia.
Katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia, Hamashauri ya wiaya Biharamulo Chama Cha Mapinduzi kilifanikiwa kupata madiwani wote kwa kata 17, huku mbunge wa jimbo hilo akishinda kwa zaidi ya asilimia 70%.