Spika Mteule wa Bunge, Job Ndugai akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 Jijini Dodoma.
Spika Mteule wa Bunge, Job Ndugai akiapa kiapo cha Uspika mara baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 Jijini Dodoma.
Spika Mteule wa Bunge, Job Ndugai akipokea katiba na kanuni kutoka kwa Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai mara baada ya kuapa kuwa Spika wa Bunge la 12 Jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge wa muda, Mhe. William Lukuvi
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
……………………………………………………………….
Na Alex Sonna,Dodoma
BUNGE la 12 limemchagua Job Ndugai kuwa Spika kwa kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa sawa na asilimia 99.7.
Ikitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi wa Spika Steven Kagaigai amesema kuwa katika ya kura hizo kura moja ilikiwa ya hapana.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa Spika Ndugai amewataka wabunge kuhakikisha wanawatumikia wananchi kama walivyoomba.
Hata Ndugai amewaambia wabunge kuwa kazi waliyonayo katika Bunge la 12 siyo kazi nyepesi maana licha ya kuwa wabunge wengi ni wa kutoka CCM lakini yanatarajiwa matokeo chanya zaidi kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Naomba niwaambie tuna kazi kubwa ya kufanya ,Bunge hili kazi haitakuwa nyepesi ,lazima liwe Bunge lenye matokeo chanya ,
” Ni kweli wabunge wengi wanatoka CCM lakini haimaanishi litakuwa Bunge la ndio tu au hapana tu ,bali linapaswa kuwa Bunge la kutekeleza wajibu wake ipasavyo.”alisema Ndugai
Ndugai amesema kuwa bunge hilo halitakuwa na kambi rasmi ya upinzani kwa kuwa hawajatimiza 12.5% . ya wabunge wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Aidha Ndugai amesema kuwa wabunge wa upinzani ambao wapo bungeni watapata nafasi sawa na hakutakuwa na ubaguzi wala upendeleo
Ametumia fursa hiyo pia kuwataka wabunge wasome kanuni za Bunge kwani hawawezi kufanya lolote bila kuzijua kanuni hizo.