NA DENIS MLOWE,IRINGA
ALIYEKUWA mtia nia wa ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM na kushika nafasi ya pili, Nguvu Chengula amesema kwamba anguko la upinzani nchini katika uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 28 mwaka huu wasitafute mchawi bali hawakusoma alama za nyakati kwani hawakuwa na ajenda ambayo ingeweza kuwashawishi wananchi kuwachagua.
Akizungumza na wanahabari, Chengula alisema kuwa wapinzani walikuja mizaha yao waliyozoea bila kubaini kuwa hali ya mambo imebadilika kutokana na kazi zilizofanywa Rais wa awamu ya Tano John Magufuli kuonekana kwa jamii ya watanzania.
Alisema kuwa wananchi wa Tanzania walipooenda kupiga kura waliangalia mengi mazuri ambayo Rais Magufuli aliyafanya hivyo alipokuwa akipiga kura alijua wa kumpa nani kwani waliamua kuchagua maendeleo yanayoonekana kuliko maneno mengi ambayo wapinzani wamekuwa wakiyatoa bila kuwa na ajenda za maendeleo kwa wananchi.
Alisema kuwa mtu ambaye amepata huduma katika kituo cha afya,katika kata , amepata umeme kijijini kwake, amefutiwa kero ya kodi ya mazao na serikali ya Magufuli angewezaje kumchagua Lissu na ajenda zake zisizo na maana na kuacha kumchagua Rais aliyemletea maendeleo ya nchini kwa kipindi kifupi.
Aliongeza kuwa ushindi wa kishindo aliopata Rais Magufuli ulikuwa dhahili tangu alipoingia madarakani ya uongozi wake kwani umegusa Maisha ya watu moja moja, amekuwakiongozi wa watu, ametatua shida za watu kuanzia mtu mmoja mmoja hadi kiwango cha Taifa hivyo ushindi huo ulitarajiwa .
Chengula alitoa wito kwa wananchi kutotishika na kelele zinazopigwa na watu wasiotakiwa mema nchi ya Tanzania kwani lazima walalamike kwani waliwaaminisha mabeberu kuwa watashinda hivyo wakawezeshwa fedha nyingi ambazo wamekosa majibu na kuwataka wapambanen na hali zao.
“ Rais Joh Pombe Magufuli ametenda kazi iliyotukuka kitu pekee alichostahili ni kutendewa sawasawa na matendo yake , kipimo kilekile cha heshima na maendeleo alichowapimia watanzania ndicho wamempimia kipimo cha kujaa na kushindiliwa hadi kumwagika cha kura nyingi” alisema
Aidha aliwataka wananchi kutokubaliana na maneno ya wapinzani kuingia kwenye maandamano ambayo lengo ni kuwaingiza watu madarakani ambao wala hawakubaliki na waroho wa madaraka na kuwataka kudumisha umoja wa Taifa na kulinda amani ya nchi kwani kipindi cha uchaguzi kimekwisha ni wakati wa kazi tu.