Rodrygo akishangilia baada ya kutokea benchi na kuifungia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 80 ikiwalaza Inter Milan 3-2 kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stefano Jijini Madrid. Real Madrid ilitangulia kwa mabao ya Karim Benzema dakika ya 25 na Sergio Ramos dakika ya 33, kabla ya Inter Milan kuzinduka kwa mabao ya Lautaro Martinez dakika ya 35 na Ivan Perisic dakika ya 68. Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi nne sawa na Shakhtar Donetsk, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na BorussiaMönchengladbach, wakati Inter Milan inaendelea kushika mkia kwa pointi zake mbili baada ya kila timu kucheza mechi tatu PICHA ZAIDI SOMA HAPA
REAL MADRID YAFUFUKA LIGI YA MABINGWA YAITANDIKA 3-2 INTER MILAN
By Alex Sonna
November 4, 2020 | 8:20 am

Related Stories
View all
Michezo
2 days ago
betPawa YADHAMINI LIGI YA KIKAPU DAR ES SALAAM KWA SH. 588.9 MILIONI
Meneja wa Kanda ya Kusini na Mashariki ya Afrika wa betPawa, Bwalya Noah akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa msimu wa wa 2026 wa…
Michezo
2 days ago
ARGENTINA NA ENGLAND KUMINYANA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA
Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa Uswisi mabao 3-1 katika mchezo wa…
