Rodrygo akishangilia baada ya kutokea benchi na kuifungia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 80 ikiwalaza Inter Milan 3-2 kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stefano Jijini Madrid. Real Madrid ilitangulia kwa mabao ya Karim Benzema dakika ya 25 na Sergio Ramos dakika ya 33, kabla ya Inter Milan kuzinduka kwa mabao ya Lautaro Martinez dakika ya 35 na Ivan Perisic dakika ya 68. Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi nne sawa na Shakhtar Donetsk, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na BorussiaMönchengladbach, wakati Inter Milan inaendelea kushika mkia kwa pointi zake mbili baada ya kila timu kucheza mechi tatu PICHA ZAIDI SOMA HAPA