WACHEZAJI wa Liverpool wakimpongeza mwenzao, Diogo Jota baada ya kufunga mabao matatu dakika za 16, 33 na 54 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya wenyeji, Atalanta kwenye mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Gewiss Jijini Bergamo. Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Mohamed Salah dakika ya 47 na Sadio Mane dakika ya 49 na kwa ushindi huo Liverpool inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Kundi D kwa pointi tano zaidi ya Ajax inayofuatia baada ya kila timu kucheza mechi tatu PICHA ZAIDI SOMA HAPA