Mgombea wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga Ahmed Salum (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28,2020 baada ya kupata kura 68,066 akifuatiwa na Washington Kasonzo (CHADEMA) aliyepata kura 11,785, Aloyce Shija (CUF) kura 1,111 na Leonard Kitile (NCCR – Mageuzi) kura 526.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Solwa Hoja Mahiba amesema waliondikishwa kupira kura katika jimbo la Solwa ni 190,962,waliopiga kura ni 83,040,kura halali ni 81,488 na kura zilizoharibika ni 1552